MSANII wa muziki Bongo, Khadija Maige ‘Kadja Nito’
amenaswa na Mapaparazi wetu akiingia nyumbani kwa sangoma aliyefahamika
kwa jina la Kimweri aliyewahi kuripotiwa kumng’arisha msanii mwenzake
Menina Attick ‘Menina Ladiva’ kisanaa.
Msanii wa muziki Bongo, Khadija Maige ‘Kadja Nito’ akiwasili kwa sangoma huyo.
Chanzo chetu cha kuaminika kilichopo jirani na eneo hilo kilieleza
kuwa kimekuwa kikimshuhudia msanii huyo akifika mahara hapo kufuata
matibabu huku dhumuni likiwa ni kusaka umaarufu ili awe staa mkubwa wa
muziki kama walivyo wasanii wengine wenye majina makubwa Bongo.
“Kuna yule msanii alitamba na kibao chake cha Maumivu, mara kwa mara
huwa anafika kwa huyu Dk. Kimweri muda wa jioni, nikifuatilia mazungumzo
yao kikubwa anachomlalamikia mganga wake huwa ni kusaka usupastaa na
jana nilimsikia akisema anaweza kufika leo jioni,” alisema sosi huyo.
Kadja Nito akiwa na sangoma huyo baada ya kuwasili.
Baada ya kupata taarifa hizo mapaparazi wetu walitinga eneo hilo na
kuweka kambi jirani na nyumba ya mtaalamu huyo na kukaa zaidi ya saa
moja wakiangaza huku na huko, mishale ya saa kumi na mbili jioni ndipo
msanii huyo alionekana akishuka kwenye Bajaj akiwa amevalia baibui na
ushungi, kisha sangoma huyo akajitokeza kumpokea wakatokomea ndani bila
kujua walipigwa picha.
Kutokana na ishu hiyo gazeti hili lilimtafuta Kadja, alipoulizwa
alionyesha mshtuko na kukiri kufika kwa sangoma huyo ambaye alidai
alikwenda kumsabahi kwa sababu wanafahamiana na si kufuata tiba.
Mtaalamu huyo alipovutiwa waya ili kutaka kujua lengo la msanii huyo
kufika ofisini kwake alijibu kwa kifupi: Nashindwa kukizungumzia hicho
mnachohitaji sababu siruhusiwi kutoa siri za wateja wangu.”
إرسال تعليق