Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Liberatusi Sabas amekanusha uvumi ulioenea
katika mitandao ya jamii kuhusu kukamatwa mwanaume mmoja aliyevalia vazi
la baibui akiwa na bomu mkoani humo na kwamba watu wengine wanne wamekamatwa wakijiandaa kuingia chuo cha uhasibu.
Uvumi
huo umeanza kusambaa kwa kasi leo asubuhi ukidai kukamatwa
kwa watu wanne waliokuwa ndani ya gari aina ya Toyota Premio
huku wakiwa na bunduki 4 aina ya SMG na Risasi 160.
Ujumbe
huo ulidai kuwa watu hao walikamatwa jana usiku wakijiandaa
kuingia chuo cha Uhasibu Arusha (IAA) kuonana na ndugu yao
mmoja wa kike anayeishi katika hosteli za chuo hicho.
Pia ilielezwa kuwa, baada ya kufika getini,mlinzi aliwashtukia na kupiga simu polisi ambapo walikamatwa.
Mbali
na taarifa hizi kukanushwa na kamanda wa Polisi,Mpekuzi
imeongea na Raisi wa wanafunzi wa Chuo hicho ndugu Iman Mkumbo
ambaye naye amezikanusha taarifa hizo na kusema si za kweli.
"Hali
ni shwari hapa chuoni,tangu juzi usiku kuna doria kali ya
polisi maeneo yote ya chuo, hivyo watu wanapata hofu na kuanza
kuzusha taarifa zisizo za kweli."Amesema Mkumbo
إرسال تعليق