Mbunge wa Maswa Magharibi (CHADEMA), John Shibuda amekataa kuhusishwa na
Chama cha Alliance for Change and Transparency (ACT-Tanzania), akisema
hana mpango wa kujiunga nacho.
Shibuda ambaye ameshatangaza kutogombea ubunge kupitia CHAsdemA katika
uchaguzi mkuu wa mwaka huu, amesema “Pamoja na kusema sitagombea kupitia
CHADEMA lakini nisilishwe maneno…siendi kwenye chama hicho cha ACT.”
Kauli ya Shibuda imeondoa uvumi ulioenea kwamba angejiunga na ACT baada ya kuwa kwenye mgogoro kwa muda mrefu na CHADEMA.
Akichangia hoja ya muswada wa sheria ya makosa ya mtandao bungeni wiki
iliyopita, Shibuda alitumia dakika mbili kuweka sawa uvumi huo akisema,
“sitaki kusemewa…nitasema mwenyewe kuhusu mstakabali wangu kisiasa. Huu
ni uzandiki.”
Hii si mara ya kwanza kwa Shibuda kuhusishwa na mpango wa kuhamia katika
vyama vingine vya upinzani. Mwishoni mwa mwaka jana pia kulikuwa na
uvumi kwamba yuko kwenye mazungumzo ya kukinunua Chama cha TADEA
kinachoongozwa na Lifa Chipaka.
Hata hivyo, Shibuda alikanusha uvumi huo akisema analishwa maneno
Post a Comment