KUHUSU WANAFUNZI WANAOLALA CHINI SEKONDARI YA MBALATSE MAKETE, MBUNGE DKT BINILITH MAHENGE AMEAMUA HIVI

Mbunge wa jimbo la Makete Dkt Binilith Mahenge akiwa katika ziara yake katika kijiji cha Kisasatu kata ya Mbalatse wilayani Makete

Na Eddy Blog
Suala la wanafunzi wa shule ye sekondari Mbalatse kulala chini kutokana na ukosefu wa vitanda katika bweni la wanafunzi shuleni hapo limeonekana kuwa miongoni mwa kero sugu inayowaumiza kichwa wananchi wa kijiji cha Mbalatse kata ya Mbalatese wilayani Makete mkoani Njombe

Hayo yamebainika kwenye mkutano wa hadhara kati ya wananchi hao na mbunge wa jimbo la Makete ambaye pia ni waziri wa nchi ofisi ya Makamu wa rais Mazingira Dkt. Binilith Mahenge uliofanyika katika kijiji hicho ambapo pamoja na mbunge kueleza yaliyofanywa wakati wa uongozi wake lakini pia alitoa fursa kwa wananchi kutoa waliyonayo

Pamoja na kueleza kero mbalimbali zinazowakumba lakini hawakusita kusema jinsi wamekuwa wakiumizwa na kitendo cha wanafunzi kulala chini kutokana na ukosefu wa vitanda kwenye bweni la sekondari yao ya Mbalatse na kusema wao kama wananchi wameshiriki kikamilifu katika ujenzi wa bweni hilo isipokuwa wamekwama vitanda

Akijibu hoja hiyo Mh Mahenge ameahidi kuleta vitanda vyote vya bweni hilo ili kuondokana na kero hiyo na kusema kuwa hakuwa na taarifa za tatizo hilo tangu awali kwa kuwa angelipatia ufumbuzi mapema iwezekanavyo

“Kwa kweli niwe muwazi hapa, hili la watoto wetu wa sekondari kulala chini limenigusa, na sijui ni kwa nini taarifa hizi hazijafikishwa kwangu mapema na viongozi wa kata, lakini hata hivyo si mbaya naomba niahidi hapa mbele yenu kwamba kuna wafadhili wamenipa msaada wa madawati 300 na kwa awamu hii hapa wanatengeneza 100 nitawataarifu wapunguze kwenye haya madawati 200 wanipe vitanda vyote vya hii sekondari, halafu na madawati mengine yatakayobakia baada ya kutengeneza vitanda

Katika hatua nyingine Dkt Mahenge amewataka viongozi mbalimbali wa kata hiyo kutobaki kimya pindi wanapokumbana na changamoto, na badala yake wawe wepesi wa kutoa taarifa maramoja kwa ngazi ya wilaya ambapo ni rahisi kumfikia yeye ili atoe ushirikiano wake mapema katika kuzitatua kero hizo na si kusubiri mpaka wananchi waje kuziibua kwenye mikutano mbalimbali anayoifanya.

Post a Comment

Previous Post Next Post