Serikali
ya Kenya imeitetea idara yake ya usalama kufuatia shutma kwamba
ilichelewa kukabiliana na shambulio la chuo kikuu cha Garissa ambapo
takriban watu 150 waliuawa.
Shambulio hilo lilisitishwa baada wapiganaji wanne waliohusika kuuawa na maafisa wa polisi saa 15 baada ya kuvamia chuo hicho.
Lakini naibu wa rais William
Ruto anasema kuwa kundi la kwanza la polisi liliwasili katika chuo hicho
saa moja baada ya shambulizi.
Amelipongeza jeshi la Kenya KDF kwa
kile alichokitaja kua hatua za haraka.Lakini vyombo vya habari vimekuwa
vikisema kuwa vikosi maalum vilivyowaua wapiganaji hao vilichelewa
kufika katika eneo hilo kutokana na mfumo wa usafiri waliotumia.
Pia kuna madai kwamba maafisa
wa polisi walifeli kuchukua hatua za dharura baada ya kupewa habari
kwamba mmoja ya wauaji ambaye sasa ametambuliwa kama Abdirahim Abdullahi
ni wakili na mwana wa chifu mmoja katika eneo la kazkazini mashariki.
Post a Comment