U-15 YAINGIA KAMBINI
Timu
ya Taifa ya Tanzania ya Vijana wenye umri chini ya miaka 15 (U-15)
imeingia kambini leo katika hoteli ya Itumbi iliyopo magomeni chini ya
kocha mkuu Adolf Rishard kujiandaa na progamu ya vijana kuwania kufuzu
kwa fainali za U-17 mwaka 2017 nchini Madagascar.
Akiongea
na waadishi wa habari leo kwenye ukumbi wa habari wa TFF Karume,
mwenyekiti wa kamati ya soka la vijana Bw. Ayoub Nyenzi amesema kamati
yake imeandaa programu maalumu ya kuwaanda vijana kwa ajili ya kuichezea
timu ya Taifa U-17 mwaka 2017.
TFF
imeandaa program hiyo ya vijana U-15 ambao watakua kambini kwa muda
siku 10, wakifanya mazoezi uwanja wa Karume na kucheza michezo kadhaa ya
kirafiki na timu za Azam U17 na shule ya Sekondari Makongo.
Kocha
mkuu na timu yake ya U-15 atazunguka mikoa saba nchini kwa ajili ya
kucheza michezo kadhaa ya kirafiki na kungamua vipaji vingine kwa ajili
ya kuboresha timu yake. Mikoa itayotembelewa ni Mbeya, Mwanza, Morogoro,
Arusha, Tanga, na Dar es alaam (Ilala, Kinondoni, Temeke).
Aidha
katika kuhakikisha timu hiyo inakua tayari kwa michuano ya kuwania
kufuzu kwa fainali za U-17 mwaka 2017 nchini Madagascar, timu hiyo ya
vijana itafanya ziara ya mafunzo mwezi Disemba mwaka huu katika nchi za
Malawi, Zambia, Zimbambwe, Botswana na Afrika Kusini kwa kucheza michezo
ya kirafiki.
Mwezi
Februari 2016 timu hiyo itacheza michezo miwili ya kirafiki na timu za
mikoa ya Dodoma na Mwanza, kabla ya kuelekea tena katika ziara kwenye
nchi za Burundi, Rwanda, Uganda na Kenya mwezi Aprili 2016.
Ratiba
ya CAF kuwania kufuzu kwa fainalizaAfrika 2017 inatarajiwa kuanza mwezi
Juni 2016, ambapo kikosi cha Tanzania kitakua kimeshapata muda mzuri wa
maandalizi kwa lengo la kuhakikisha timu inashiriki fainali hizo nchini
Madagascar 2017.
Fainali
za U-17 mwaka 2017 zinatarajiwa kufanyika nchini Madagascar, huku
Tanzania ikitarajia kwa kuwa mwenyeji wa fainali hizo za vijana U-17
kwa mwaka 2019.
Jumla ya wachezaji 30 wameitwa kuingia kambini, wachezaji hao ni Kelvin
Deogratius, Magazi Dotto, Anthon Shilole (Geita), Sadik Sud Ramadhani ,
Mwinchumu Yahya(Tanga),Faraji John, David Mbakazi , Juma Juma, Pius
Raphael, Davison Meddy, Maulid Lembe (Dodoma), Ibrahim Koba (Morogoro).
Wengine
ni Abubakar Badru Nassoro, Yusuf B.A. Khalfani, All Hafidh Mohamed
(Kusini Pemba), Joachim Mwenda, Charles Cassiano, Luqman Shauri (Tanga),
Juma Zuberi (Kigoma), Ismail Abdallah (Kusini Pemba), Robert Philipo
(Arusha), Alex Peter, Mohamed Ally, Rashid Kilongola (Kinondoni), Saad
Juma (Mkoa Magharibi), Ibrahim Shamba (Kusini Unguja), Ally Msengi,
Klevin S.Kijili (Mwanza), Frank Abel (Simiyu) na Bryan Jamal.
VPL KUENDELEA KESHO
Ligi
kuu ya Vodacom Tanzania inatarajiwa kuendelea kesho jumatano katika
viwanja viwili jijini Dar es salaam, kwa vinara wa ligi hiyo Young
Africans kuwakaribisha Coastal Union kwenye dimba la Uwanja wa Taifa.
Uwanja
wa Chamazi Complex, wenyeji timu ya Azam FC wanaokamata nafasi ya pili
kwenye msimamo wa Ligi Kuu, watawakaribsiha wagonga nyundo kutoka jijini
Mbeya timu ya Mbeya City FC.
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
Post a Comment