KIMENUKA! Siku chache baada ya habari ya staa wa
Bongo Fleva anayesumbua na wimbo wa Shikorobo, Nurdin Bilal ‘Shetta’
kudaiwa kulala chumba kimoja na mwigizaji Rose Ndauka kuandikwa
gazetini, mkewe Neila Yusuf ameshindwa kuvumilia na kudai talaka yake,
Risasi Mchanganyiko linakujuza.
Staa wa Bongo Fleva anayesumbua na wimbo wa Shikorobo, Nurdin Bilal ‘Shetta’ akiwa na mkewe.
Alhamisi iliyopita, Shetta na Rose waliripotiwa na gazeti ‘dugu’ na
hili la Amani kuwa walilala katika chumba kimoja katika Hoteli ya
Kingway iliyopo mkoani Morogoro walipokuwa wamekwenda kwenye mazishi ya
muasisi wa Kundi la Tip Top Connection, Abdul Bonge.
Kwa mujibu wa chanzo makini, mara baada ya gazeti hilo kusambaa
mtaani na mke wa Shetta kufikishiwa nakala yake na wapenda ‘ubuyu’,
kilinuka ile mbaya nyumbani kwa Mbongo Fleva huyo, Kijitonyama jijini
Dar ambapo mwanamke aliamua kudai talaka yake.
Mke huyo wa Shetta ambaye wamebahatika kupata mtoto mmoja na msanii
huyo (Kayla) alimjia juu mumewe na kutaka amwambie ukweli wa habari hiyo
jambo lililoleta tafrani hadi kufikia hatua ya kutimka nyumbani hadi
wazazi wa pande zote mbili wakalazimika kuweka vikao vya usuluhishi.
Licha ya jitihada hizo kutoka kwa wazazi, bado mama Kayla alikataa
kusuluhishwa na kudai hasira zake zitashuka mara atakapokutana na Rose
uso kwa uso.“Kilinuka kiasi cha mke wa Shetta kufungasha virago huku
akisisitiza kwamba kabla ya kuondoka mazima atahakikisha anamfungia kazi
Rose ili aweze kumweleza kinaga ubaga juu ya ilikuwaje akapindua na
mumewe chumba kimoja,” kilisema chanzo.
Mwigizaji Rose Ndauka.
Wanahabari wetu walimtafuta Rose na kumuuliza kama amepata taarifa za
kutafutwa na mke wa Shetta na kuhusu kuhusishwa na tukio hilo ambapo
alijibu kuwa hajapata taarifa.“Mimi sijapata hizo taarifa, kama
ananitafuta mimi nipo tu maana sijafanya kosa lolote. Kama nilivyosema
awali, kweli nilisafiri na Shetta kwenda Morogoro na tulilala hoteli
moja lakini vyumba tofauti, Shetta namheshimu siwezi kufanya naye jambo
kama hilo,” alisema Rose.
Mapaparazi wetu baada ya kumalizana na Rose, walimvutia waya Shetta
ili kujua ukweli wa tukio hilo ambapo alikiri kumtokea na kuwashushia
lawama wambeya.“Ni kweli mke wangu amekerwa sana na habari zile, kuna
wambeya ndiyo wamemjaza maneno kiasi cha kuleta tafrani hadi wazazi
kuingilia kati ingawa mimi naamini haya ni mambo ya kifamilia tu ambayo
mke wangu atayaelewa na yataisha tu.
“Mke wangu ni muelewa sana, nampenda na ananipenda, hii hali ni ya
kawaida kwa wanandoa ila kwa kuwa mimi ni msanii mke wangu atajua tu
kuwa watu wanaongea sana juu yetu,” alisema Shetta.
Post a Comment