MTANGAZAJI
mkongwe wa televisheni, Sauda Mwilima ambaye mumewe, Kauli Juma
aliondoka mara tu baada ya kufunga naye ndoa kuelekea Afrika Kusini
kikazi, amesema wa ubani wake huyo amesharejea na hivyo kuwakejeli
waliokuwa wakisema kuwa ndoa yao ilikuwa ni magumashi.
Mtangazaji mkongwe wa televisheni, Sauda Mwilima.
Akipiga stori na paparazi wetu, Sauda alisema kwa sasa anaifurahia
ndoa yake vilivyo baada ya mumewe kurudi Bongo baada ya kuwa Afrika
Kusini kikazi kwa muda mrefu na baadhi ya watu kuzungumza mengi kuhusu
ndoa yao.
“Nadhani watu sasa watajua kuwa siyo jambo zuri kuzungumzia kitu
usichokijua, mume wangu amerudi na hakuna ninachokifurahia kama ndoa
yangu. Ama kweli ndoa ni tamu,” alisema Sauda.
Post a Comment