show
 ya mwisho kufanya na marehemu sharo ilikuwa mwembe yanga show ya DTV.. 
nakumbuka ilikuwa inaitwa "NI WAKATI WAKO TOUR" baada ya hapo kesho 
asubuhi tukaenda tanga kushoot movie yetu hii ambayo 20/04/2015 ndio 
inatoka.. tukamaliza kushoot salama salimini tukarudi DAR.. usiku 
napigiwa simu na marehemu sajuki anataka niende kwenye show yake iringa 
CHANGIA SAJUKI.. tarehe 25/11/2012 Sharo akabaki kwa sababu alikuwa 
katoka magomeni kaamia sinza na ana siku mbili kw hyo bado mgeni sinza..
 basi mm nikafanya show ya marehemu sajuki vzr tu, tarehe 26 wasanii 
tunarudi kutokea iringa kuja dar kwenye msiba wa marehemu JOHN MAGANGA..
 pia nae alikuwa msanii mwenzetu, nafika ubungo simu yng inaita 
naangalia sharo.. nikapokea akaniuliza vp bado mpo mbali nikamjibu nipo 
ubungo akaniambia hata mm pia nipo ubungo naelekea Tanga kumuona mama.. 
jibu langu nikamuambia ww si tumetoka tanga hata wiki bado na hvyo c 
unajua kwmba tunamsiba wa msanii mwenzetu... jibu lake Sharo  akaniambia
 kuna jambo muhimu hata na ww mwenyewe shuka uje twende wote coz ni 
jambo muhimu sana plz...!! wakati mm nahangaika kutafuta wap gari yke 
ipo kwa muda nikawa siioni lakini yy ananiona, kumbe mwenzangu kaacha 
OPA kachukua gari nyngne ya mudy suma.. taa zinaruhusu sharo anatupita..
 na  kwa ukatuni wake sharo tunapishana sauti ya mwisho kwa kumuona 
macho kwa macho aliniambia "say.. ooh mamaaa...!!" Nafika msibani kwa 
John maganga tumbo likanza kuniuma nikapitiliza home moja kwa moja punde
 sms inaingia kutoka kwa sharo, broo sipo poa nahisi km nimerogwa hivi..
 hayo yalikuwa maneno yake mwisho kupitia sms.. kuanzia hapo  tumbo 
likaanza kuchanganya kuuma mpaka saa mbili na dakika zake.. napigiwa 
simu ya msiba wa sharo.. Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema 
peponi Aameen...!! na kuanzia hapo ndio nikajua kwa nini sharo alikuwa 
ananilazimisha tuwe na @stanbakora
 ktk kazi zetu..?? ilikuwa sio rahisi kiivyo mm kumuelewa ingawaje kumbe
 mwenzangu alikuwa anamanisha... kwa hyo show ya mwisho kufanya na 
marehemu Sharo Milionea ilikuwa MWEMBE YANGA na show ya kwanza kufanya 
na @stanbakora ilikuwa MWEMBE YANGA ya 
E.fm
E.fm
.jpg)
إرسال تعليق