IMELDA MTEMA
MSANII wa sinema za Kibongo, Brenda Malembeka 
‘Kunguru’ ameibuka na kuanika ukweli wa maisha yake kuwa kabla ya kutoka
 kisanaa, aliteseka sana kwa kutumwa pombe na wasanii waliokuwa tayari 
na majina makubwa.
Akizungumza na mwanahabari wetu, Kunguru alisema kwa kipindi hicho 
ilimlazimu akubali kutumwa pombe na mastaa kwani lengo lake lilikuwa ni 
kupatiwa nafasi ya kucheza uhusika ukuu. “Nilikubali sana kutumwa pombe 
na mastaa wakubwa ili lengo langu litimie, nashukuru Mungu kwa sasa 
nimepata shavu kwenye filamu inaitwa Asante iliyoandaliwa na Masai Media
 Group,” alisema Kunguru.
إرسال تعليق