Kwenye show ya LEO TENA ambayo huwa
inasikika #OnAiR kila siku on @CloudsFM huwa kunakua na Hekaheka pia..
zinatoka mtaani kwenye maisha ya kawaida ya kila siku yani, iliyosikika
leo ni mwendelezo wa kilichosikika jana, mwanamke mmoja kaolewa mara
mbili, yani katoka kwenye ndoa ya kwanza kwenda kwa mwanaume mwingine.
Kilichosikika jana ni kwamba mvulana
ambaye alimuoa mara ya pili alisema kwamba mwanamke huyo alimdanganya
kwamba anasoma kidato cha tatu, wakaendelea na uhusiano mpaka wakafikia
hatua ya kuoana, masheikh walishtukia katikati ya shughuli kwamba
mwanamke huyo ameolewa na ana watoto wanne, leo aliyesikika kwenye
Hekaheka ni mume wake wa kwanzaanasimulia jinsi ambavyo mke wake
aliondoka.
Mwanaume huyo amesema hawakuwahi kuwa na
ugomvi siku za nyuma, alishangaa kuona mke wake anadai talaka ghafla
bila sababu, baadae akasikia kwamba ameolewa na mwanaume mwingine.
Mume huyo amesema kamsamehe lakini
hayuko tayari kurudiana nae.. Mwanamke huyo alikoolewa ndoa
haikukamilika, masheikh waliizuia kutokana na mwanamke huyo kushtukiwa
kwamba hakufuata taratibu ili aolewe ndoa ya pili.
Najua utakua na hamu kumsikia mwanaume huyo akiongelea ishu ya kuachana kwao, bonyeza play hapa uisikie Hekaheka yote..
إرسال تعليق