Lowassa akiri taasisi nyingi nchini kukosa fursa za ajira.

Waziri mkuu wa zamani, Edward Lowassa.
Waziri mkuu wa zamani, Edward Lowassa,  amekiri kuwapo kwa changamoto ya ajira kutokana na taasisi nyingi kukosa nafasi za ajira nchini.
Amesema suala la ajira linahitaji ufumbuzi wa hali ya juu ili wahitimu mbali mbali wanaomaliza vyuo vikuu kunufaika na  kuondokana na umasikini, ikiwamo kushirikiana na sekta binafsi katika kukuza soko la ajira.
Lowassa aliyasema hayo juzi wakati wa hafla  ya sherehe ya kutumiza miaka 60 ya Naibu Waziri wa Kazi na Ajira, Dk. Mkongoro Mahanga, yeye akiwa ndiye mgeni rasmi.
Lowassa alitoa wito kwa wazazi nchini kuwekeza kwenye elimu kwa watoto na vijana wao ili taifa liliweze kuwa na wasomi wengi ambao watakuja kuisaidia nchi kupata watalaamu kwenye nyanja mbalimbali.
Alisema kuwekeza kwenye elimu kwa watoto ni uwezekaji ambao utakuja kusaidia familia kwa mambo mbalimbali ikiwemo ujasiliamali pamoja na kupata viongozi walio bora wanaotegemewa na taifa.
Aidha, aliwataka vijana kuwa na malengo na kulipa kipaumbele suala la elimu kwani ndiyo msingi imara hata kuwapata wanasiasa ambao watalisaidia taifa hili kulipeleka mbele katika maendeleo.
Alisema katika kukabiliana na tatizo hilo ni kuongeza shule za awali hadi elimu ya juu ikiwa ni sehemu pekee ya kulisaidia taifa. 
Kwa upande wake, Dk. Mahanga,  amemhakikishia Waziri Mkuu huyo wa zamani kuendelea kukabiliana na changamoto za ajira ikiwa ni pamoja na kutatua matatizo ya ajira nchini na kutoa kipaumbele kwa vijana wa kizalendo kadri ajira zinavyopatikana.
Alisena serikali itaendelea kushirikiana na taasisi binafsi katika kukabiliana na changamoto za ajira.

Post a Comment

أحدث أقدم