Staa wa filamu Bongo, Lungi Maulanga hivi karibuni ametoa ushuhuda
wake kwamba alikuwa akisumbuliwa na tatizo la kujisaidia kitandani mpaka
alipofika kidato cha pili lakini alipona katika mazingira ya
kushangaza.
“Niliposhuka, akaniambia nibadili nguo na kusema tatizo langu limeisha, sikuamini lakini ukweli ni kwamba kuanzia siku hiyo sikujisaidia tena kitandani.”
Staa wa filamu Bongo, Lungi Maulanga.
Akizu-ngumza Lungi alifunguka: “Nikiri tu kwamba nilikuwa
kikojozi mpaka nafikia form two, nilikuwa naona aibu sana lakini
aliyenisaida ni bibi mmoja ambaye aliniponya katika mazingira ya
kushangaza.“Baada ya kumwambia tatizo langu, aliniambia nipande kwenye
mti wa muembe nikiwa na nguo zangu, nikiwa juu akaniambia nikojoe kisha
nishuke.“Niliposhuka, akaniambia nibadili nguo na kusema tatizo langu limeisha, sikuamini lakini ukweli ni kwamba kuanzia siku hiyo sikujisaidia tena kitandani.”
Post a Comment