Na Editha Karlo, Globu ya Jamii - Kigoma
MKAZI
wa Kijiji cha Buzebazeba katika Manispaa ya Kigoma Ujiji, Zuwena Abdu
(29) jana amejifungua watoto mapacha wanne kwa mkupuo katika Hospital ya
Mkoa wa Kigoma (Maweni).
Zuwena
alisema kuwa watoto aliojifungua wenye jinsi ya kiume ni watatu na
mmoja ambaye ni wa mwisho ana jinsi ya kike ,wa kwanza akiwa na uzito
wa kilo 1.8,pili 2.5 wa tatu 1.7 na wanne 1.7.
Alisema watoto hao alijifungua jana majira ya saa kumi na mbili jioni salama kwa njia ya kawaida
Zuwena
alisema huo ni uzazi wake wa tano ambao awali alijifungua wanne kwa
njia ya kawaida kwahiyo jumla anaidadi ya watoto nane.
''Kwanza
nina mshukuru mungu kwa kuniwezesha kujifungua salama watoto wote na
wakiwa hai kutokana na hali duni ya kiuchumi ya familia yetu mimi na
mume wangu tunaomba Watanzania wenye mapenzi mema watusaidie ili tuweze
kuwalea hawa watoto,mume wangu hana kazi na mimi sina kazi''alisema mama
huyo
Muuguzi
wa zamu katika wodi ya wazazi Agness Nguvumali alisema kuwa
alifikishwa mama huyo alifikishwa hospitalini hapo siku ya jumatatu saa
kumi jioni akiwa na uchungu na ilipofika saa kumi na mbili akawa
amejifungua mapacha wanne kwa njia ya kawaida salama.
Muuguzi
huyo alisema kuwa watoto wote wana afya njema alisema wataendelea
kubaki hospitalini hapo kwaajili ya uangalizi wa karibu wa madaktari.
Agness
amewaomba Watanzania,mashirika mbalimbali kujitokeza kumsaidia mama
huyo ili aweze kuhudumia watoto wake hao kwakuwa hali yake ya uchumi na
mume wake siyo nzuri na utunzaji wa mapacha hao unahitaji uwezo wa nguvu
ya ziada.
YEYOTE MWENYE MSAADA KWA WATOTO HAO ANAWEZA KUWASILIANA KWA KUTUMIA NAMBA 0752202783
Mama wa watoto mapacha wanne, Bi. Zuwena Abdu akiwa wodini baada ya kujifungua.
Muuguzi
wa zamu katika Wodi ya wazazi ya Hospital ya Mkoa wa Kigoma (Maweni),
Agness Nguvumali akiwaangalia mapacha wanne waliozaliwa hospitalini
hapo.
Post a Comment