Akizungumza leo jijini Dar es salaam, Rais wa Simba Evans Aveva alisema kuwa chini ya uongozi wake wameanzisha tuzo hizo kwa wachezaji wa Simba ili kuibua morali ya wachezaji na kuthamini mchango wao na hiyo imekuja baada ya klabu hiyo ya wekundu wa Msimbazi kuingia mkataba wa miaka mitano na Kampuni ya EAG ambao watakuwa na jukumu la kuiwezesha Simba kupata mapato kwa njia mbali mbali ikiwemo udhamini kutoka makampuni mbali mbali.
Aveva
alisema pia mbali na kumpa gari mchezaji bora wa klabu hiyo pia
kutakuwa na tuzo ya mchezaji bora anayechipukia, kiungo, mshambuliaji
bora na mchezaji mwenye nidhamu.
"Mchezaji bora atapata gari, mchezaji bora chipukizi atapata Sh5 milioni waliosali watapata Sh2 milioni ikiwemo mwenye nidhamu.
Aveva alisema pia mbali na
tuzo hizo pia watatoa tuzo ya mchezaji aliyetukuka 'All Fame' ambaye nae
atapata kiasi hicho cha fedha na pia mbali na zawadi hizo wachezaji hao
watapewa simu aina ya Huawei.
Mbali na tuzo hizo Aveva
alisema pia Kampuni hiyo ya EAG itakuwa pia na jukumu la kuhakikisha
Simba inafanikiwa mikakati yake ya kuongeza mapato, kukuza namba ya
wanachama, kuongeza na kuwapa faida wanachama wa Simba kupitia huduma za
Bima, kuongeza ari ya wachezaji Simba, kuwaenzi na kukumbuka wachezaji
wa zamani.
"Lengo la utekelezaji wa
mikakati hii ni kukuza ajira kutokana na biashara zitakazoanzishwa,
tunaamini tukitumia bidhaa za Simba ambazo tunalenga kuzifikisha kila
sehemu Tanzania na kutengeneza mfomo wenye lengo la kuuipatia mapato
stahiki tofauti na sasa.
"Kupitia mkakati huu Simba
itakuwa na uwezo wa kujenga uwanja wake na kuwa na vyanzo endelevu vya
mapato vitakavyoiwezesha kuboresha kiwango cha timu na kuifanya iwe bora
si Tanzania pekee bali Afrika nzima....: "Kwa timu yenye mamilioni ya
washabiki hili si jambo lisilowezekana bali linalowezekana, ni jambo la
kufurahisha na kuona uongozi wa Simba umetambua hili."alisema Aveva.
Naye mkurugenzi wa EAG Group
Iman Kajura akizungumzia suala hilo alisema "Kupitia mkataba huu
nataka kuona Simba inapata mabadiliko makubwa ya kiuchumi kwa kuitafutia
vyanzo vingi vya mapato, ili iache kutegemea mapato ya mlangoni na ada
za wanachama pekee."
Kajura alisema mipango yote
ya kuendesha zoezi hilo anaipata kutoka klabu ya Arsenal ya England
ambayo anafanya nayo kazi katika kukuza na kuingiza wabia wa biashara.
HABARI NA MICHUZI BLOG
Post a Comment