Na Victor Mariki – Ofisi ya Makamu wa Rais.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Maku wa Rais - Mazingira, Mh.
Binilith Mahenge (pichani), amezindua Kanuni mpya ya Mazingira itakayodhibiti uchafuzi wa
mazingira unaotokana na makelele yanayosabishwa na shughuli mbalimbali katika
jamii .
Akizungumza katika uzinduzi wa Kanuni hizo jijini Dar es Salaam, Mh. Mahenge alisema
kuwa Ofisi yake ilishazitangaza Kanuni hizo katika Gazeti la Serikali tangu
tarehe 30/01/2015 kulingana na Sheria ya Usimazi wa Mazingira ya mwaka 20104.
Aidha Mh. Mahenge aliongeza
kuwa Sheria hiyo ya Mazingira ya mwaka 2004 iliyoanza kutumika
rasmi tarehe 1 Julai, 2015 inaiwezesha Ofisi yake kuandaa na kuunda kanuni
mbalimbali za mazingira ili kudhibiti uchafuzi wa mazingira nchini.
Hata hivyo alifafanua kuwa kanuni mpya za kudhibiti kelele,
hazitadhibiti kelele zitokanazo na ving`ora vya magari ya Polisi, magari ya
zimamoto, magari ya kubebea wagonjwa pamoja na
mizinga wakati wa magwaride katika sherehe za kitaifa.
Kanuni hizi zimeundwa kuitikia wito wa malalamiko kutoka kwa
wadau mbalimbali waliokuwa wakiilalamikia serikali kuhusu uchafuzi mkubwa wa
mazingira unaotokana na kelele katika kumbi za starehe, uchimbaji wa madini
pamoja namitetemo inayosabishwa na minara ya simu.
Post a Comment