Kamishna
wa Forodha na Ushuru kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Tiagi
Masamaki Kabisi akiwaeleza waandishi wa Habari juu ya faida za Mfumo
mpya wa Uondoshaji Mizigo bandarini(TANCIS) ikiwa unasaidia katika
kufanya makadirio ya kodi sahihi kulingana na taarifa sahihi zilizoletwa
kwa kutumia mfumo huo, pia utasaidia wateja kujua sehemu mizigo yao
ilipo na pia wanapaswa kulipa kiasi gani kulingana na mzigo wa mteja,
wakati wa Mkutano na waandishi wa Habari leo Jijini Dar es Salaam.
Kaimu
Meneja wa Kituo cha Huduma cha Forodha kutoka Mamlaka ya Mapato
Tanzania (TRA) Bw. Kasty Phelician akiwaeleza waandishi wa Habari
majukumu ya kituo hicho ikiwemo kutoa tathnimi ya kodi unayopaswa
kulipwa kwa kupitia na kuhakiki nyaraka zote kutoka kwenye kadhia
zinazotumia mfumo wa TANCIS ikiwamo viwango vya ushuru wa forodha
vinavyopaswa kutozwa.
Meneja
wa Forodha Bandari ya Dar es Salaam kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania
(TRA)Bw.Burton Kaissy akiwaeleza waandishi wa Habari namna
wanavyoshirikiana na Taasisi mbalimbali kurahisisha usafirishaji wa
mizigo yote inayoenda nje nchi.
Baadhi
ya waandishi wa Habari wakimsikiliza Meneja wa Forodha Bandari ya Dar
es Salaam kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)Bw.Burton Kaissy wakati
wa Ziara iliyofanyika katika mamlaka hiyo kuona jinsi mfumo wa TANCIS
unavyofanya kazi.(PICHA NA HASSAN SILAYO-MAELEZO).
Post a Comment