Maajabu! Msichana aliyefahamika kwa jina la Dora mkazi wa Magomeni
Bagamoyo mkoani Pwani, hivi karibuni amejikuta akijifungua nazi badala
ya mtoto, jambo lililomshangaza kila mtu.
Ushirikina watajwa
Ushirikina watajwa
Dora anayedaiwa kujifungua nazi.
Ilidaiwa kuwa, chanzo cha Dora kujifungua nazi ni maneno aliyoambiwa
na mke mwenzake aliyefahamika kwa jina la Jamila ambapo aliambiwa
hatajifungua kiumbe cha kawaida na ndipo alipokimbilia Dodoma kukwepa
matatizo.
Msikie Dora
Msikie Dora
Akizungumza na Amani hivi karibuni akiwa nyumbani kwake Bagamoyo, Dora alisema:
“Nilihamia Bagamoyo nikitokea Mwanza, nikakutana na mwanaume anayeitwa Pascal, tukakubaliana tuishi kama mke na mume.
“Nilihamia Bagamoyo nikitokea Mwanza, nikakutana na mwanaume anayeitwa Pascal, tukakubaliana tuishi kama mke na mume.
“Baada ya kukubaliana hilo, nikapata ujauzito lakini nikashangaa siku
moja akaja mwanamke na kusema yeye ni mzazi mwenzake na
Pascal.“Alifanya vurugu, akanijeruhi kisha akachukua TV na vitu vingine,
akaondoka huku akiniambia lazima nijifungue kiumbe cha ajabu. Nilipata
hofu kubwa, mara nikaanza kusumbuliwa na tumbo, nikapelekwa kwa mganga
ambapo niliambiwa nimerogwa.
Mume wa Dora akihojiwa na mwandishi wa habari (hayupo pichani)
“Nikatibiwa kisha nikafungwa kitambaa chenye dawa mkononi na kuambiwa
nisikivue. “Siku moja kikapotea kimaajabu, baadaye tukakiona juu ya mti
nje ya nyumba. Nikaachana na masuala ya kienyeji, nikaamua kwenda
kanisani, hata hivyo mauzauza hayakuisha,” alisema Dora na kuongeza:
“Siku uchungu uliponijia nikiwa Dodoma, ndugu zangu na wakunga wakaja
kunisaidia lakini cha ajabu wakashangaa kuona nazi ndiyo
inatoka.“Wakakimbia na kuniacha nikipandisha mashetani, akaitwa mganga
wa kienyeji lakini naye aliogopa ndipo nikapelekwa kwa walokole
kuombewa.
“Nilipopata nafuu na kurudishwa nyumbani, polisi wakaja na kutuambia
eti tumetupa mtoto, wakasachi hawakuona kitu, wakatupeleka kituoni.“Huko
nako nikapandisha mashetani, nilipotulia nikapelekwa hospitali ambako
nilisafishwa lakini ishu ikawa kubwa, polisi wakatuchukua mimi na mume
wangu na kutuweka ndani, tulitoka baada ya kutoa pesa.
Mfano wa nazi aliyojifungua Dora.
“Cha ajabu niliporudi nyumbani ili nichukue kadi niende kliniki,
nikakuta shanga kibao, ndipo tukaona cha msingi ni kurudi Bagamoyo na
kuhama pale tulipokuwa tunaishi,” alisema Dora huku akiungwa mkono na
mumewe, Pascal.
Imeandaliwa na Chande Abdallah na Deogratius Mongela
إرسال تعليق