Cake
maalum iliyoandaliwa kwenye sherehe za uzinduzi wa shamra shamra za
miaka 70 ya Umoja wa Mataifa uliofanyika mwishoni mwa juma kwenye hoteli
ya White Sands jijini Dar es Salaam.
Mratibu
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la
Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (katikati)
akiteta jambo na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la UN
Women nchini Tanzania, Anna Collins kabla ya zoezi la kuwasha mishuma 70
kwenye cake hiyo ikiwa ni uzinduzi wa shamra shamra za miaka 70 ya
Umoja wa Mataifa. Kushoto ni Mshehereshaji wa sherehe hizo Afisa Habari
wa kituo cha habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Usia Nkhoma Ledama.
Mratibu
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la
Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (wa pili
kulia) na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la UN Women
nchini Tanzania, Anna Collins wakiwa wamejumuika na wafanyakazi wa
mashirika ya Umoja wa Mataifa kwenye mnuso huo.
Mratibu
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la
Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (wa pili
kushoto) akiwasha nakshi nakshi zilizowekwa kwenye cake maalum ya
uzinduzi wa shamra shamra za miaka 70 ya Umoja wa Mataifa nchini.
Anayemkingia upepo ni walioandaa Cake hiyo kutoka kampuni ya M.E Gift
Wraps and Delivery huku Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa
la UN Women nchini Tanzania, Anna Collins naye akijianda kufanya zoezi
hilo.
Wafanyakazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini wakishiriki kuwasha mishumaa 70 iliyowekwa kwenye cake hiyo.
Wafanyakazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa wakikata cake kwa niaba ya wafanyakazi wenzao.
Mratibu
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la
Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (kulia)
akila kipande cha cake kwenye mnuso huo.
Wafanyakazi
wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini Tanzania wakilishana cake kabla
ya kupata chakula cha usiku wakati wa shamra shamra za uzinduzi wa
miaka 70 ya Umoja wa Mataifa.
Mtaalam
wa Mahusiano na Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania, Hoyce
Temu (kushoto) akibadilishana mawazo na wafanyakazi wenzake.
Pichani
juu na chini ni wafanyakazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini
wakijumuika kwenye chakula cha usiku wakati wa sherehe za uzinduzi wa
shamra shamra za miaka 70 ya Umoja wa Mataifa Tanzania.
Mratibu
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la
Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akifuatiwa
na Afisa Habari wa UNIC, Usia Nkhoma Ledama wakipakua chakula cha jioni
kwenye mnuso huo.
Pichani juu na chini ni wafanyakazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa wakijisevia nyama choma ndani ya hoteli ya White Sands.
BAADA YA KUPATA BUFEE LA NGUVU ULIWADIA ULE WASAA WAKUFANYA DIGESTION YA CHAKULA KWA KUSAKATA RHUMBA…
Wafanyakazi
wa mashirika ya Umoja wa Mataifa wakisakta rhumba kwenye hafla ya
uzinduzi wa shamra shamra za miaka 70 ya Umoja wa Mataifa nchini.
Wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa wakionyesha ufundi wa kusakata rhumba kwenye mnuso huo.
Mratibu
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la
Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (mwenye
shati ya kijivu) naye hakubaki nyuma alionyesha umahiri wake.
Mwakilishi
Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la UN Women nchini Tanzania, Anna
Collins naye alionyesha ufundi wake kama anavyoonekana pichani.
Usia Nkhoma Ledama naye akasema hata wasinichezee hawa…. akajibu mapigo.
Burudani ikiendelea kwa furaha kabisa na amani.
Huku couple hii ikisakata Zouk rhumba.
Mdogo mdogo ya Diamond nayo ilihusika.
Mduara nao ulihusika.
Mtaalam
wa Mahusiano na Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania, Hoyce
Temu akiteta jambo na majaji wa shindano la kucheza muziki kwa
wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa wakati wa mnuso huo.
Baadhi
ya wafanyakazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa walioingia fainali
kwenye mashindano ya kucheza wakionyesha umahiri wao mbele ya majaji
(hawapo pichani).
Majaji wakiwa kwenye wakati mgumu wa kutafuta mshindi kwa washiriki.
Pichani juu na chini ni mchuano ukiendelea kwa Top 3.
Na
huyu ndio aliibuka mshindi wa kwanza, pichani akionekana kutoka nje ya
dancing floor na kuzunguka bustani nzima na couple yake huku wafanyakazi
wenzao wakiwashangilia.
Chief Judge Laurean Kiiza wa UNIC na timu yake ya majaji wakitangaza washindi.
Mshindi
wa kwanza akionyesha mbwembwe zake mbele ya Mratibu Mkazi wa Mashirika
ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la
Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez kabla ya zoezi la picha ya
pamoja.
Mratibu
mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la
Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez katika
picha ya pamoja na majaji pamoja na TOP 3 kwenye mashindano ya kusakata
rhumba.
Mratibu
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la
Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akiteta
jambo na mmoja wa wanakamati wa shughuli hiyo Yona Samo wa UNDP mara
baada ya kumalizika kwa sherehe hiyo iliyofungwa na shindano la muziki.
إرسال تعليق