Goli la kwanza la Yanga katika DK ya 2 tu ya mchezo lilifungwa kwa njia
ya penati baada ya Msuva kufanyiwa madhambi ndani ya 18. Na naodha wa
Yanga Canavaro akakwamisha wavuni mpira huo kama unavyoona golikipa
Etoile akipishana nao na kudaka upepo.
Mchezaji wa Timu ya Etoile Du Sahel ya Tunisia, Bounedjah Baghdad
akiangalia namna ya kuwatoka wachezaji wa Yanga, Mbuyu Twite na Amissi
Tambwe wakati wa mchezo wa Kimataifa wa Kombe la Shirikisho unaoendelea
kupigwa hivi sasa kwenye uwanja wa Taifa, jijini Dar es salaam. Kipindi
cha pili kimeanza hivi punde na matokeo ni 1-1.Picha zote na Othman
Michuzi.
Mshambuliaji wa Yanga, Mrisho Ngassa akiruka daluga la Beki wa Timu ya
Etoile Du Sahel ya Tunisia wakati wa mchezo wa Kimataifa wa Kombe la
Shirikisho unaoendelea kupigwa hivi sasa kwenye uwanja wa Taifa, jijini
Dar es salaam. Kipindi cha pili kimeanza hivi punde na matokeo ni 1-1.
Wachezajiwa Timu ya Yanga, wakishangilia ushindi sambamba na mashabiki wao.
Kiungo wa Timu ya Etoile Du Sahel ya Tunisia, Franck Kom aruka juu
kuwania mpira wa kichwa wakati wa mchezo wa Kimataifa wa Kombe la
Shirikisho unaoendelea kupigwa hivi sasa kwenye uwanja wa Taifa, jijini
Dar es salaam. Kipindi cha pili kimeanza hivi punde na matokeo ni 1-1.
CREDIT:JIACHIE
إرسال تعليق