MSUTO! Mwanamke aliyetajwa kwa jina la Sina, mkazi wa Kawe jijini Dar amejikuta akisutwa mchana kweupe baada kumvujishia taarifa rafiki yake aitwaye Cheka Komba Mbegere kuwa wanawake wanaojiita Cash Money wanakwenda kumsuta, Risasi Mchanganyiko lilifuatilia hatua kwa hatua.Mwanamke aliyetajwa kwa jina la Sina (mwenye nguo nyekundu mbele kushoto), mkazi wa Kawe jijini Dar akisutwa mchana kweupe na wanawake wanaojiita Cash Money wanakwenda kumsuta.
Tukio hilo lilitokea hivi karibuni ambapo Cash Money walichoshwa na
tabia ya umbea wa Cheka ambaye ni memba wa kundi hilo, ndipo walipoamua
kumfungia kazi lakini akanusurika baada ya kutonywa na Sina ndipo wamama
hao waliobeba ngoma za vidumu vya maji walipomsuta Sina kwa niaba ya
Cheka.
Kwa mujibu wa Jamila ambaye naye ni memba wa Cash Money, Cheka
alimgombanisha yeye na Sheila kwa kumwaambia kuwa wanatembea na bwana
mmoja aitwaye Bubu pasipo kujijua.“Huyu mama amenifanyia kitu mbaya
sana, alikuwa anakwenda kumwambia Sheila kuwa mimi natembea na mume wake
ambapo tulikuwa tukigombana mara kwa mara na mwisho ndiyo hiyo juzi
aliponivamia na kunipiga wakati nimelewa.
Majibizano yakendelea.
“Kwenye ule ugomvi Cheka naye alikuja kunichangia, kesho yake
nilipozinduka nilikwenda kituo cha polisi Kawe na kushtaki, asivyo na
haya akamuandikia SMS Sheila akimwambia waende kwa mganga ili eti
waifute kesi,” alisema Jamila.
Baada ya kuona mambo yameshindakana kwa mganga, Sheila akaona bora
amuombe msamaha Jamila ndipo walipomjua ‘mchawi’ wao ni Cheka kisha
wakaungana kwenda kumsuta.
“Nilipoona mambo yamenifika shingoni nikaona nirudi kwa mwenzangu
nimuombe msamaha tupatane, ndiyo nikamweleza mtu aliyekuwa
akituchonganisha tukapanga siku ya kumsuta ambayo ndio leo lakini bahati
yake akawa ametonywa akakimbia, tulichunguza tukabaini ametonywa na
Sina ndipo naye tukamsuta barabara,” alisema Sheila.
Paparazi
wetu aliwashuhudia Cash Money wakimuimbia Sina nyimbo za kumsuta huku
wakipiga ngoma za vidumu vya maji kwa takriban nusu saa ambapo Sina
alileta vurugu kali ya kutaka kujinasua lakini hakufanikiwa.
“Hii ndiyo kiboko ya wambeya, kwa aliyeona fedheha hii kamwe hawezi kufanya umbeya wa aina yoyote,” alisikika shuhuda mmoja.
“Hii ndiyo kiboko ya wambeya, kwa aliyeona fedheha hii kamwe hawezi kufanya umbeya wa aina yoyote,” alisikika shuhuda mmoja.
Baada ya kumalizika kwa tukio hilo, paparazi wetu alimvutia waya
Cheka ili kumuuliza kama ni kweli alihusika kuwagombanisha Jamila na
Sheila na sababu za yeye kutimka nyumbani hapo siku ya tukio.“Mimi
nilikimbia kwa sababu walisema eti wamewaita waandishi waje wanisute
lakini ukweli ni kwamba mimi sijawahi kuwachonganisha ila walipopigana
nilikwenda kuwasuluhisha.
“Hata
hivyo wale hawanipendi kwa sababu nimejitoa kwenye kundi lao na
ninawadai hela zangu ndio maana wananichafua,” alisema Cheka. Hata
hivyo, Cash Money waliahidi kufanya msuto ‘party two’ muda wowote
watakapomtia mikononi Cheka wakidai wamechoshwa na tabia yake ya
kuwagombanisha watu.
إرسال تعليق