Mara baada ya kuelezwa kwamba wapo kwenye uhusiano wa kimapenzi huku
wenyewe wakidanganya wana ‘projekti’, hatimaye majirani wamefichua kuwa
mwigizaji Shamsa Ford na mwanamuziki Emmanuel Elibariki ‘Nay’, sasa
wanaishi kama mke na mume.
Mwigizaji Shamsa Ford na mwanamuziki Emmanuel Elibariki ‘Nay’ wakizungumza jambo.
Baada ya kutonywa ‘mchapo’ huo, gazeti hili liliwadamkia nyumbani
kwa Nay maeneo ya Kimara-Korogwe jijini Dar na kumkuta Shamsa akiwa na
kanga moja.Mwanahabari wetu, baada ya kufika nyumbani hapo mishale ya
asubuhi alikuwa bega kwa bega kuwafuatilia ambapo alifanikiwa kugundua
kwamba wawili hao sasa wanaishi kama mume na mke.
Habari zilizopatikana zilidai kwamba, kwa sasa Shamsa hana muda
mwingi wa kukaa nyumbani kwake kwani asilimia tisini kama si mia moja
kabisa, anautumia kukaa na Nay nyumbani hapo.Mara kadhaa mwandishi wetu
amekuwa akifika nyumbani hapo na kumkuta Shamsa akipika na kupakua huku
akiwa na kanga moja huku wenyewe wakiitana mke na mume na kuoneshana
mahaba motomoto.
...Wakipozi kimahaba.
“Kwani tatizo lipo wapi? Siwezi kufanya siri tena, sisi tupo kwenye
uhusiano wa kimapenzi kama unavyotuona, nimeamua kumchagua Nay kwa kuwa
anajua kupenda na kuthamini,” alisema Shamsa alipohojiwa na paparazi
wetu.
Alipoulizwa Nay kulikoni ‘kumficha’ Shamsa nyumbani kwake, alifunguka:
Alipoulizwa Nay kulikoni ‘kumficha’ Shamsa nyumbani kwake, alifunguka:
“Yeah! Kwa sasa hakuna project tena, hapa ni mapenzi kwa kwenda
mbele, sipendi kuwazungumzia wengine, napenda kuangalia uhusiano wangu
upo vipi kwa sasa, ninampenda Shamsa.”
...Wakipata msosi.
Nay na Shamsa walianza uhusiano huo mara baada ya mwanamuziki huyo
kudai kwamba alimnasa mpenzi wake, Siwema akiwa na mwanaume ndani ya
sita kwa sita hivyo kuamua kuachana naye moja kwa moja na kujikuta
akiangukia kwa mwigizaji huyo.
إرسال تعليق