|
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb)
akimtazama kwa furaha mmoja wa watoto yatima wanaolelewa kwenye kituo
cha Nyumba ya Furaha na Amani kilichopo Kigogo Mburahati, Jijini Dar es
Salaam. Waziri Membe alikitembelea kituo hicho wakati wa Siku Kuu ya
Pasaka. |
|
Mhe.
Membe pamoja na Mkewe Mama Dorcas Membe wakipata maelezo juu ya watoto
waishio katika kituo hich kutoka kwa Sista Mary Bakhita |
|
Mhe
Membe akizungumaza wakati wa ziara yake kituoni hapo. Kulia ni Mama
Dorcas Membe. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Mhe. Paul Makonda
akifuatiwa na Padri Timoth Maganga wa Kanisa Katoliki la Kigogo
Mburahati
|
|
Watoto yatima wakiwa na walezi wao |
|
Sehemu ya Wazee wanaolelewa na Kituo hicho wakimsikiliza Mhe. Waziri (hayupo pichani) alipowatembelea |
|
Sehemu nyingine ya Wazee na Watoto |
|
Waziri
Membe akikata keki pamoja na Sista Bakitha kama ishara ya kusherehekea
Siku Kuu ya Pasaka pamoja na Watoto Yatima na Wazee wanaolelewa kwenye
kituo cha Nyumba ya Furaha na Amani. Pembeni ni Mama Dorcas Membe nae
akifurahia |
|
Mhe. Wazriri akijumuika kwa chakula cha mchana pamoja na watoto Kituoni hapo. |
|
Watoto hao nao wakifurahia chakula cha mchana na Mgeni wa aliyewatembelea na kusheherekea nao Sikukuu ya Pasaka |
|
Waziri Membe akitoa msaada kwenye kituo hicho |
|
Waziri Membe pamoja na Mkewe Mama Dorcas Membe katika picha ya Pamoja na Masista wanaolea watoto yatima katika kituo hicho |
|
Waziri Membe akisaini kitambu cha wageni alipowasili katika kituo hicho. |
|
Baadhi ya Watoto wanaolelewa katika kituoni hapo wakitoa burudani mbele Waziri Membe (Hayupo pichani). |
|
Waziri Membe akizungumza na Waandishi wa Habari.Picha na Reginald Philip
----
|
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard Membe ametoa
wito kwa Watanzania kujenga utamaduni wa kuwasaidia watu wasiojiweza
waliopo kwenye jamii wakiwemo watoto yatima, walemavu, wazee na wajane.
Waziri
Membe ametoa wito huo hivi karibuni alipotembelea Kituo cha Kulelea
Watoto Yatima na Wazee cha Nyumba ya Furaha na Amani kilichopo Mburahati
Jijini Dar es Salaam.
Mhe.
Membe alisema kuwa katika jamii za watu kumekuwa na makundi ambayo
yanahitaji msaada mkubwa kutoka kwa watu wengine ambao kwa namna moja au
nyingine wamejaaliwa kipato kidogo na afya. Alisema kuwa ni wajibu wa
watu wa aina hiyo kuwasaidia wale wanaohitaji kama vile watoto yatima,
walemavu, wazee na wajane.
Waziri
Membe ambaye alikuwa amefuatana na Mke wake, Mama Dorcas Membe aliguswa
sana na historia ya baadhi ya watoto yatima aliowatembelea kituoni
wakiwemo wale waliotupwa jalalani na kuokotwa wakiwa kwenye hali mbaya.
“Lipo
kundi linalopata mateso na matatizo katika jamii zetu tunazoishi. Ni
vizuri Watanzania tukajenga utamaduni wa kutembelea sehemu kama hizi
ili kujionea wenyewe hali halisi. Kwa kweli ni hali ya kusikitisha kuona
baadhi ya watoto walitupwa na kuokotwa jalalani na wengine tayari
wakiwa wamepata majeraha ya kung’atwa na mbwa. Hivyo ni wajibu wetu sote
kuwasaidia kwa chochote kidogo tunachojaaliwa kupata”, alisema Waziri
Membe.
Aidha,
Mhe. Membe aliwapongeza na kuwasifu Masista wa Shirika la Mama Theresa
ambao ndio wasimamizi wa kituo hicho kwa kuwalea watoto, vijana na
wazee wenye matatizo mbalimbali na kuwaomba waendelee kujipa moyo katika
kazi hiyo kwani ni njia moja wapo ya kumtumikia Mungu.
Awali
akimkaribisha Waziri Membe kituoni hapo, Sista Mkuu wa Kituo hicho,
Sista Mary Bakhita, alisema kuwa wamefurahia sana ziara hiyo ya Mhe.
Membe hususan katika Siku Kuu ya Pasaka kwani ni faraja kubwa kwao kwa
Watoto na Wazee wanaolelewa kituoni hapo.
“Tumefarijika
sana kula pasaka pamoja nawe Mhe. Waziri. Watoto na Wazee hawa
wanajisikia vizuri pale wanapotembelewa na tunaomba uendelee na moyo huo
huo”, alisema Sista Bakhita.
Wakati
wa ziara hiyo Mhe. Membe na familia yake walitoa zawadi mbalimbali kwa
kituo hicho ikiwemo vyakula, sabuni na fedha kiasi cha shilingi milioni
10 kwa ajili ya kusaidia shughuli mbalimbali kituoni hapo.
-Mwisho-
إرسال تعليق