Jeshi
la polisi kanda maalumu ya Dar es salaam limesema wafuasi wa
Askofu mkuu wa kanisa la ufufuo na uzima,Josephat Gwajima
wasithubutu kutia mguu eneo atakalohojiwa askofu huyo.
Kauli ya jeshi hilo imekuja siku chache baada ya Askofu Gwajima kuwataka wafuasi wake kumsindikiza leo kituo cha polisi kanda maalumu ya Dar es salaam ambako anahitajika ili kuhojiwa.
Msimamo
huo ulitolewa juzi na kamshna wa polisi katika kanda hiyo,
Suleiman Kova wakati akizungumza na mtandao huu ambapo
alisisitiza kuwa anayehitajika kufika katika kituo hicho ni
Gwajima na mwanasheria wake.
Kamishna
Kova alisema ni vema wafuasi hao wakaendelea na kazi zao za
uzalishaji,kwani kwenda kituoni hapo bila mwito au kukamatwa ni
kosa.
Kova
alisema eneo hilo haliruhusiwi watu kukusanyika, hivyo kwa
usalama wao ni vyema wakaendelea na shughuli zao na kuliacha
jeshi hilo lifanye mahojiano na Askofu huyo wakiwa huru.
"Napenda
kutumia nafuasi hii kumuomba Gwajima awaambie wafuasi wake
hawahitajiki kufika eneo hilo kwani anayehitajika ni yeye na
mwanasheria wake," alisema Kova.
Kova
alisema iwapo kila mtu atafuata taratibu hakuna nguvu
itakayotumika kutoka jeshi la polisi, lakini endapo watakiuka
hakuna njia mbadala ambayo inaweza kutumika zaidi ya kutumia
nguvu.
Kauli
ya Kova inakuja kutokana na kauli ya Gwajima aliyoitoa
wakati wa sikukuu ya pasaka kuwataka wafuasi wake kujitokeza
katika kituo hicho wakati atakapokwenda kuhojiwa.
Gwajima
alisema lengo la kuwataka wafuasi hao kujitokeza ni ili
waweze kujua kila kitu kinachoendelea katika sakata hilo kwani
kuna taarifa ambazo zimekuwa zikizushwa na watu kupitia
mitandao mbalimbali.
Akizungumzia
hali ya usalama katika jiji la Dar, Kova alisema ni shwari
na kuahidi kuwa wanaendelea na oparesheni ya kukamata wauza
dawa za kulevya, wahalifu na kulinda maeneo ya fukwe.
Pia,
alisema wamejipanga kukabiliana na vitendo vya kigaidi ambapo
wanafanya uchunguzi kila mahali kwa kutumia vikosi vya mbwa,
farasi,helkopta, magari, pikipiki na kutembea kwa miguu katika
maeneo yote ya jiji
إرسال تعليق