POMBE si chai! Msemo huu ulitimia hivi karibuni
baada ya staa wa filamu za Kibongo, Salma Jabu ‘Nisha’ kuzidiwa na
kilevi na kuanza kushindana kukata mauno na kusababisha azingirwe na
wanaume waliovutiwa naye.
Staa wa filamu za Kibongo, Salma Jabu ‘Nisha’ akikata mauno.
Tukio hilo la aina yake lilitokea Jumatano iliyopita katika sherehe
ya bethidei ya mtoto wa msanii mwenzake, Halima Yahya ‘Davina’
iliyofanyika katika viwanja vya Hoteli ya Lamada jijini Dar ambapo
kulikuwa na vyakula na vinywaji vikali vya kila aina.
Nisha ambaye alikuwa amevalia kikaptula cha ‘jeans’ na kujistiri na mtandio, baada ya kukolea ulevi aliutupa mtandio na kuacha sehemu kubwa ya mwili wazi kisha kukata mauno kushindana na mademu mcharuko waliokuwa ukumbini hapo kiasi cha kuwapagawisha wanaume wakware ambao walimvaa na kutaka kucheza naye.

Davina akiwa na mwanaye.
“Duh yaani Nisha leo ametia aibu, si kawaida yake nahisi mitungi
imemzidi. Ameamua kujiachia kupitiliza, hebu mwangalie anavyokata mauno
watoto wanamuangalia, aibu hii,” alisikika mualikwa mmoja akimwambia
mwenzake.
Mauno mauno.
Hata hivyo, Davina alipoona baadhi ya waalikwa wanazidisha kusaula na
kukatika, aliomba kipaza sauti na kuwataka wasifanye hivyo kwani
sherehe ni ya mtoto.Sherehe hiyo ilihudhuriwa na mastaa kibao akiwemo
Jeniffer Kyaka ‘Odama’, Mayasa Mrisho ‘Maya’, Mike Sangu, Steven
Mengere ‘Steve Nyerere’ na wengine wengi ambao baadhi yao walionekana
wakiwa wamekolea kilevi.
Post a Comment