Serikali
ya Kenya imemtambua mmoja ya wapiganaji waliohusika katika mauaji ya
chuo kikuu cha Garissa kwamba ni mtoto wa afisa wa serikali.
Msemaji
wa wizara ya ndani amesema kuwa Abdirahim Abdullahi ni miongoni mwa
watu wanne walioshambulia chuo kikuu cha Garissa siku ya alhamisi na
kuwaua watu 148.
Mtu huyo sasa ametambulika kama mwana wa kiume wa Chifu wa eneo la Kazkazini mashariki mwa kenya.
Alidaiwa kutoweka na ilihofiwa kwamba amesafiri nchini Somalia.
Wizara ya ndani inasema kuwa wapiganaji wote waliuawa siku ya alhamisi.
Washukiwa
wengine watano wamakamatwa kufikia sasa kwa kuhusishwa na mauaji hayo
ambayo ni mabaya zaidi kuwahi kutekelezwa na kundi la wapiganaji wa
Alshabaab.
Post a Comment