Serikali yapewa mabilioni kuboresha bandari

Dar es Salaam. Zaidi ya Sh 1.2 trilioni zimetolewa na wadau wa maendeleo kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maboresho ya Bandari ya Dar es Salaam inayofanywa chini ya Mpango wa Matokeo Mkubwa (BRN)sasa.
Miradi hiyo ambayo utekelezaji wake utaanza kesho itafanywa kwa awamu mbili ambapo inatarajiwa kukamilika ndani ya mwaka huu na mwaka ujao.
Akizungumza lleo kwa niaba ya Waziri wa Uchukuzi, Samuel Sitta, wakati wa uzinduzi utekelezaji wa awamu ya kwanza ya miradi hiyo Katibu Mkuu wa wizara hiyo Dk Shaaban Mwinjaka amesema, fedha hizo zitatumika kwenye miradi ya maboresho ya miundombinu ya bandari.
Amesema, sekta ya uchukuzi hasa bandari inakuwa kwa kasi hivyo miundombinu yake lazima iboreshwe ili iende sambamba na mabadiliko hayo.
“Tunataka ifikapo 2020 bandari iwe na uwezo wa kuingiza mizigo kutoka tani milioni 13 hadi tani 22 milioni.”
Amesema, fedha zilizotolewa na wadau hao zitatumika kwa mgawanyo kulingana na miradi.
“Utekelezaji wa awamu ya kwanza ambayo ni kubomoa ghala mbili za bandarini na kuboresha barabara  ndani ya bandari umefadhiliwa na TradeMark Africa (TMEA).”amesema
Ameongeza, “Awamu ya pili itafadhiliwa na Benki ya Dunia (WB) pamoja na Idara ya Maendeleo ya Kimataifa (DFID).”
Akizungumzia mchango wao Mkurugenzi Mtendaji wa TMEA, David Stanton amesema, wametoa Sh 108 bilioni kwa ajili ya kubomoa ghala hizo.
“Fedha hizo zitasaidia kwenye kazi iliyoanza leo ambayo itaendelea hadi mwezi ujao kwa ajili kuboresha eneo hili ambalo litaanza kutumika kama sehemu ya kuweka kontena na siyo ghala tena.”amesema Stanton.
Naye, mwakilishi kutoka WB Monthe Biyoud amesema, benki yao pamoja na DFID watatoa Sh 873 bilioni kwa ajili ya utekelezaji mradi wa awamu ya pili.
Amesema hadi kufukia Desemba mwaka huu wanatarajia fedha hizo zitakuwa zimeshatolewa.

Post a Comment

Previous Post Next Post