Kocha mkuu wa Simba, Goran Kopunovic.
WAKATI Ligi Kuu Bara inaelekea ukingoni, Kamati ya Usajili ya Simba, tayari imeanza kufanya tathmini ya wachezaji inaowahitaji kuongeza nguvu kwa ajili ya msimu ujao.
Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe,
aliliambia Championi Jumamosi kuwa, “Siwezi kukuambia majina, lakini
tutaongeza wachezaji katika nafasi tatu kwa ajili ya kujiimarisha
zaidi.“Kwanza ni beki wa kati, tunalazimika kujiimarisha zaidi kutokana
na tulivyoona utendaji katika nafasi hiyo.
“Hatujajua beki atatokea nje au ndani ya Tanzania, tayari tumeanza
kutafuta taratibu. Pili tunahitaji kiungo ambaye atakuwa na uwezo wa
kukaba na kuchezesha timu ili kusaidiana na kina (Said) Ndemla na (Abdi)
Banda pale kati.
“Nafasi ya tatu ni mshambuliaji, ukiangalia inaonyesha wazi tunahitaji mtu mzuri wa kufunga,” alisema Hans Poppe.Alisisitiza watakaa na Kocha Goran Kopunovic na kusikia ana maoni au mapendekezo yapi.
“Nafasi ya tatu ni mshambuliaji, ukiangalia inaonyesha wazi tunahitaji mtu mzuri wa kufunga,” alisema Hans Poppe.Alisisitiza watakaa na Kocha Goran Kopunovic na kusikia ana maoni au mapendekezo yapi.

إرسال تعليق