Amejibu mapigo? Baada ya staa wa sinema za Kibongo, Shamsa
Ford kuhamia kwa mwanamuziki Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’,
aliyekuwa mwandani wa jamaa huyo, Siwema Edson naye amevunja ukimya kwa
kumwanika mwanaume wake ikidaiwa ndiye yule aliyefumaniwa naye.
Habari kutoka jijini Mwanza anakoishi Siwema maeneo ya Kitangiri
zilidai kwamba kitendo cha Nay kutundika mitandaoni picha za mahaba
akiwa na Shamsa ndicho kilichomfanya mwanadada huyo naye kujibu mapigo.
Habari zilieleza kwamba Siwema amekuwa akionekana na jamaa huyo (wengine wanamwita Serengeti boy) katika viunga mbalimbali vya starehe jijini humo na klabu iliyopo ndani ya Hoteli ya Golden Crest.
Ilidaiwa kwamba, baada ya Siwema na jamaa huyo kujipiga picha kwa kutumia simu za viganjani ndipo wakazitupia mtandaoni bila kusema chochote.
Picha hizo ambazo Ijumaa Wikienda linazishikilia, zinawaonesha wawili hao wakiwa kwenye mahaba mazito huku wakibusiana midomoni na kushikana maeneo hatarishi.
Watu wake wa karibu wanadai kuwa Siwema ameshindwa kuvumilia na kuamua kumwanika jamaa huyo ili ‘kama mbwai, mbwai tu’.
Baada ya kunyetishiwa na kuona picha zao za kimahaba, gazeti Ijumaa wikienda hili lilimtafuta Siwema kwa njia ya kilongalonga akiwa jijini Mwanza ‘Rocky City’ ambapo alikiri kuwa huyo jamaa ni mtu wake.
“Yes (ndiyo). Kweli hizo picha ni zangu na huyo ni mtu wangu.
“Kwa taarifa yako dawa ya moto ni moto,” alisema Siwema kisha akakata simu akimaanisha kuwa hataki maswali zaidi.
Machi 15, mwaka huu maeneo ya Kitangiri jijini Mwanza, Nay alidai kumfumania Siwema na Serengeti boy ambapo msanii huyo alimnyang’anya mwanadada huyo mtoto waliyezaa pamoja kisha akazama kwenye penzi la Shamsa.

إرسال تعليق