
Baada ya hapo naanza kupiga simu ya Hussei Machozi inaita
lakini haipokelewi kwa zaidi ya nusu saa, naanza kupata wasiwasi,
nikiwatafuta rafiki zake pia sifanikiwi lakini baadae naendelea kuipiga
simu ya Hussein na inapokelewa.

Katika picha zilizosambaa na kumuhusisha Hussein Machozi, hii ni mojawapo.
Sauti ni ya Hussein mwenyewe, anaanza kwa kusema ‘Nilijiandaa
hapa nimekwenda mazoezini kucheza mpira, niliacha simu yangu kwenye
charge na niliporudi baada ya mazoezi nakuta missedcalls nyingi sana,
msg na simu za mama yangu pamoja na dada, wakati najiandaa kuanza kupiga
simu ghafla naanza kupata simu za watu mbalimbali kwamba nimepata ajali
na kufariki, mimi nikawaambia sio kweli mimi ni mzima na nipoDar es salaam‘
Kumbe
baada ya taarifa za kifo kusambaa na kuwafikia Mama yake mzazi pamoja
na dada yake ambao walipiga simu yake na haikupokelewa kwa muda mrefu,
wakaamini kweli kilichotokea ni kifo…. mama akazimia hapohapo, dada akaanguka na kuzimia vilevile.

Mama anaendeleaje? ni yapi mengine ameyasema Hussein Machozi? bonyeza play hapa chini kumsikia mwenyewe…
habari hii ni kwa mujibu wa millardayo.com
Post a Comment