Ni jioni ya Jumatano ya April 15 2015 nipo
 ofisini na naanza kupokea simu nyingi za watu wangu wakitaka kujua 
ukweli kuhusu taarifa zilizoenea kwamba msanii wa bongoflevaHussein Machozi amefariki kwenye ajali iliyohusisha gari la mizigo na gari dogo Dodoma.
Baada ya hapo naanza kupiga simu ya Hussei Machozi inaita
 lakini haipokelewi kwa zaidi ya nusu saa, naanza kupata wasiwasi, 
nikiwatafuta rafiki zake pia sifanikiwi lakini baadae naendelea kuipiga 
simu ya Hussein na inapokelewa.

Katika picha zilizosambaa na kumuhusisha Hussein Machozi, hii ni mojawapo.
Sauti ni ya Hussein mwenyewe,  anaanza kwa kusema ‘Nilijiandaa
 hapa nimekwenda mazoezini kucheza mpira, niliacha simu yangu kwenye 
charge na niliporudi baada ya mazoezi nakuta missedcalls nyingi sana, 
msg na simu za mama yangu pamoja na dada, wakati najiandaa kuanza kupiga
 simu ghafla naanza kupata simu za watu mbalimbali kwamba nimepata ajali
 na kufariki, mimi nikawaambia sio kweli mimi ni mzima na nipoDar es salaam‘
Kumbe
 baada ya taarifa za kifo kusambaa na kuwafikia Mama yake mzazi pamoja 
na dada yake ambao walipiga simu yake na haikupokelewa kwa muda mrefu, 
wakaamini kweli kilichotokea ni kifo…. mama akazimia hapohapo, dada akaanguka na kuzimia vilevile.
Sasa
 hivi Hussein inabidi alazimike kusafiri mpaka kwao Singida Manyoni ili 
kuwahakikishia ndugu zake kwamba yuko hai manake aliongea kwenye simu ya
 kaka yake na kumpa Dada simu baada ya kuzinduka lakini dada hajaamini, kasema anafichwa tu lakini ni kweli Hussein kafariki.
Mama anaendeleaje? ni yapi mengine ameyasema Hussein Machozi? bonyeza play hapa chini kumsikia mwenyewe…
habari hii ni kwa mujibu wa millardayo.com

إرسال تعليق