Watu 10 wanashikiliwa na polisi mkoani Morogoro baada ya kukamatwa
msikitini wakiwa na milipuko 30, sare za jeshi na bendera nyeusi
inayodaiwa kutumiwa na kundi la wapiganaji wa Al Shabaab wa nchini
Somalia.
Katika tukio hilo, mmoja anayesadikiwa kuhusiana na watu hao
waliokamatwa aliuawa na wananchi wenye hasira baada ya kumjeruhi kwa
panga askari polisi aliyekuwa akipambana naye.
Akizungumza na waandishi wa habari leo, Kamanda wa polisi mkoani
Morogoro, Leonald Paul alisema tukio hilo limetokea jana (Aprili 14)
majira ya saa 3.30 usiku katika kitongoji cha Nyandero, tarafa ya Kidatu
wilayani Kilombero.Kamanda Paul alimtaja mtu aliyefariki kuwa ni Hamad
Makwendo ambaye umri wake haujafahamika ambaye ni mkazi Manyasini Ruaha
wilayani Kilombero.
Aidha alisema siku ya tukio polisi walipata taarifa kutoka kwa raia wema
kuhusu watu hao na kwamba walitaarifiwa kuwa wanajihusisha na matukio
mbalimbali ya uhalifu na polisi waliamua kufatilia nyendo zao.Akisimulia
tukio hilo, Kamanda Paul alisema: “Polisi walipata taarifa kuwa watu
hao walitumia usafiri wa bajaji mbili kwenda kusikojulikana na wakati
wakiendelea na zoezi la kufuatilia ndipo walikutana na bajaji moja ikiwa
na abiria mmoja ambaye ni Mkwendo na kuisimamisha.”
Alisema kuwa bajaji hiyo iliposimama marehemu huyo aliruka na kuanza
kukimbia ndipo askari mwenye namba F .3323 Koplo Nasoro alianza
kumkimbiza na alipomkaribia mtuhumiwa huyo alichomoa jambia alilokuwa
nalo na kumkata askari huyo eneo la shingoni.
Askari mwingine mwenye namba E.9245 Koplo Chomola ambaye alikuwa nyuma
alifanikiwa kumpiga risasi ya mguu mtuhumiwa huyo, ambapo alipoanguka
chini wananchi wa eneo hilo tayari walifika katika eneo hilo na kuanza
kumshambulia marehemu huyo kisha kumchoma moto kwa hasira.
Kamanda huyo alisema walianza kuwasaka watu wengine ambao walipata taarifa wapo katika Msikiti wa Suni uliopo Kidatu.
“Polisi walipofika katika msikiti huo waliuomba uongozi wa msikiti huo
kuwatoa watu wote waliokuwa msikitini ili kuweza kubaini watu ambao
wanatiliwa mashaka.”
Alisema polisi walendelea na ukaguzi na kuwakamata watu hao 10 wakiwa na vifaa hivyo na kuwatia nguvuni.Kamanda
huyo alitaja vitu vilivyokutwa katika mabegi yaliyokuwa ndani ya
msikiti huo ni pamoja na milipuko 30, bendera nyeusi yenye maandishi ya
Kiarabu yakisomeka ‘Mungu Mmoja’, majambia, bisibisi, vinyago vya kuziba
uso (masks), nguo
إرسال تعليق