Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini TFF Jamal Malinzi, ametuma salamu za rambi rambi kwa Rais wa klabu ya Simba SC Bw. Evans Aveva kufuatia vifo vya mashabiki wa klabu hiyo, viliyotokea jana katika ajali ya barabarani eneo la Makunganya mkoani Morogoro.
Katika
salamu zake Rais Malinzi amesema, TFF imezipokea kwa masikitiko taarifa
hizo za ajali na kwa niaba ya familia ya mpira wa miguu nchini,
wanawapa pole wafiwa wote na mwenyezi Mungu awape nguvu majeruhi waweze
kupata nafuu na kupona kwa uharaka zaidi.
Aidha
Rais Malinzi ameagiza michezo yote ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania
itakayochezwa wikiendi hii nchini, kusimama kwa dakika moja ili
kuwakumbuka mashabiki waliopoteza maisha katika ajali hiyo

إرسال تعليق