Kocha
wa Manchester United Louis van Gaal ameonya kuwa timu yake bado iko
kwenye mbio za ubingwa licha ya kuwa nyuma kwa pointi nane dhidi ya
vinara wa Ligi Kuu Chelsea.
Van Gaal pia amekiri kuwa Marouane Fellaini amekuwa nguzo muhimu kutokana na kuimarika kwa kiwango chake.
Ushindi
dhidi ya Aston Villa Jumamosi utaongeza presha kwa majirani zao
Manchester City ambao hawatacheza hadi Jumatatu pale watakapoikabili
Crystal Palace.
Van
Gaal ambaye amethibitisha kuwa Robin van Persie bado ni majeruhi,
amesema bado kuna vita vya kugombea nafasi ya nne lakini lolote linaweza
kutokea hata kwenye kuwania taji.

إرسال تعليق