Watanzania 23 waishio Afrika Kusini wamewekwa kwenye kambi
maalumu ya Isipingo nchini humo ili kupewa ulinzi wa maisha yao yaliyo
hatarini kufuatia mashambulizi yanayofanywa na wazawa dhidi ya wageni.
Watu hao ambao ndiyo idadi ya Watanzania
waliotambulika kuwa hatarini nchini humo, wanatarajia kuwasili nchini
muda wowote baada ya Serikali ya Afrika Kusini kuridhia.
Watakaorejea nchini ni Watanzania 21, wengine wawili wameomba kuendelea kubaki huko.
Watakaorejea nchini ni Watanzania 21, wengine wawili wameomba kuendelea kubaki huko.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Kimataifa, Bernard Membe alisema hakuna Mtanzania aliyepoteza maisha
katika vurugu zilizosababishwa na chuki dhidi ya wageni, lakini wapo
Watanzania watatu waliokufa nchini humo kwa sababu nyinginezo.
Membe aliwataja waliofariki kuwa ni Rashid
Jumanne. Alisema Mtanzania huyu alikuwa ni jambazi na aliuawa kilomita
90 kutoka mji wa Durban akiwa kwenye harakati zake za unyang’anyi.
Mtu wa pili alisema anaitwa Athman China. Alisema
kijana huyu aliuawa kwa kuchomwa kisu ndani ya gereza la West Hill.
Membe alifafanua kuwa China alifanya kosa la jinai akafungwa, na huko
gerezani zikatokea fujo za wafungwa. Kijana huyo alikufa baada ya
kuchomwa kisu na wafungwa wenzake.
Ally Mohamed alikuwa ni kijana wa tatu kufa akiwa
Afrika Kusini. Membe alisema Mohamed alikuwa amelazwa hospitali huko
Johanesberg kwa maradhi ya kifua kikuu.
Kijana huyo alifariki baada ya kuugua kwa miezi miwili, na tayari mwili wake umewasili nchini kwa maziko.
Kijana huyo alifariki baada ya kuugua kwa miezi miwili, na tayari mwili wake umewasili nchini kwa maziko.
“Kuna habari zimesambaa mitandaoni kwamba
Watanzania wamekufa huko Afrika Kusini. Niweke wazi kuwa hakuna
Mtanzania aliyepoteza maisha kutokana na vitendo vya chuki dhidi ya
wageni.
Mpaka sasa ni watu nane tu ndiyo waliopoteza maisha,” alisema waziri huyo na kuongeza kuwa watu hao wanatoka katika nchi za Ethiopia, Zimbabwe, Malawi na Swaziland.
Mpaka sasa ni watu nane tu ndiyo waliopoteza maisha,” alisema waziri huyo na kuongeza kuwa watu hao wanatoka katika nchi za Ethiopia, Zimbabwe, Malawi na Swaziland.
Membe alisema aliwasiliana na Waziri wa Usalama wa
Afrika Kusini, David Mahlobo akamthibitishia kuwa hakuna Mtanzania
yoyote aliyekufa.
Pia, alimwita balozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini ili aeleze zaidi madhara yaliyojitokeza kwa Watanzania waishio Afrika Kusini.
Pia, alimwita balozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini ili aeleze zaidi madhara yaliyojitokeza kwa Watanzania waishio Afrika Kusini.

Post a Comment