INATISHA!
Huku Wabongo wengi wakiendelea kukimbilia Afrika Kusini (Sauzi) kwa
kigezo cha kutafuta maisha mazuri, imethibitika kwamba hali ya amani
nchini humo si salama.
Wahamiaji wakionekana kujiokoa pamoja na watoto wao.
Kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali kutoka nchini humo, Wabongo wengi na
wageni wengine kutoka nchi tofautitofauti Afrika kama Zimbabwe,
Botswana, Namibia na nchi nyingine wamekuwa wakifanyiwa vitendo vya
kikatili na hata kuuawa na wenyeji wa nchi hiyo wakidai wanawakosesha
ajira.
“Jamani hali inatisha sana huku, wageni tunauawa sana, wengine
wanachomwa moto na kuchomwa visu hadharani, hakuna amani tena,” alisema
Mbongo mmoja anayeishi nchini humo.Chanzo kiliendelea kudadavua kwamba
Waafrika Kusini wanachukizwa na wageni hao kwani wamekuwa wakipokea
ajira kutoka kwa matajiri kiasi kwamba wao wameonekana hawafai kwani
wengi hawataki kazi ngumu tofauti na ilivyo kwa wageni ambao hupiga kazi
yoyote bila kujali ugumu wa kazi.
Wahamiaji wakiwa kwenye hifadhi baada ya kukimbia machafuko.
Imeelezwa kuwa usalama wa wageni nchini humo umekuwa mdogo mno kiasi
kwamba wengine wamekuwa wakijificha ndani kwa wiki nzima pasipo kutoka
nje kwa kuhofia kuuawa na wenyeji ambao wamekuwa wakirandaranda mitaani
kuwatafuta wageni ili wawadhuru.
“Sijatoka nyumbani wiki nzima, nipo nimejifungia tu, hata kwenda
kununua chakula inakuwa ngumu sana, jamani, chondechonde waambie
Watanzania wasikimbilie huku, hali inatisha sana,” kilisema chanzo
chetu.
Mara baada ya kusambaa kwa taarifa za mauaji yanayoendelea kutokea Afrika Kusini, Watanzania wengi wameonekana kukasirishwa na kitendo hicho hivyo kukemea vikali mauaji hayo.
Mara baada ya kusambaa kwa taarifa za mauaji yanayoendelea kutokea Afrika Kusini, Watanzania wengi wameonekana kukasirishwa na kitendo hicho hivyo kukemea vikali mauaji hayo.
“Hii
siyo fair kabisa, sifurahii kuona ndugu zetu wakiuawa huko, naomba
warudi nyumbani na hata sisi tuliokuwa hapa nyumbani tutulie tu kwani
maisha popote pale,” alisema kijana mmoja aishiye Manzese Midizini.
إرسال تعليق