Pichani ni picha ya Mtanndao ni namna ya wahalifu wa kimtadao wanavyoingilia mfumo wa computer yako na kuchukua vitu muhimu.
Jeshi
la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linawashikilia watuhumiwa
watatu raia wa kigeni kwa makosa yanayohusiana na wizi wa mtandao kwa
lengo la kuiba katika vyombo vya fedha kama mabenki, maduka ya
kubadilishia fedha (Bureau de Change) au kuingilia miamala ya fedha
zinazosafirishwa na wateja kutoka nje na ndani ya nchi.
Polisi
wa kikosi Maalum cha kupambana na wizi wa mtandao (Cyber Crime)
walipata taarifa za kuaminika kwamba watu hao watatu walikuwa katika
mazingira ya kutiliwa mashaka na ndipo Polisi walienda Mtaa wa Mindu
eneo la Upanga na kuwakamata.
Watu hao walikutwa katika nyumba namba 416 iliyopo katika ghorofa ya nne na walitambuliwa kwa majina yafuatayo: FOTIOS S/O VOGIATZIS, Miaka 32, Mfanyabiashara, Mkazi wa Upanga, Raia wa nchini UGIRIKI mwenye Passport namba AK2669977.
ATHANASIOS S/O VOGIATZIS, Miaka 30, Mfanyabiashara, Mkazi wa Upanga, Mkazi wa Ugiriki mwenye Passport namba AK3049876n na PANAGIOTIS S/O ANGELIDIS, Miaka 25, Mkazi wa Upanga, Raia wa UGIRIKI mwenye Passport namba AK2644930.
Kamanda Kova akifafanua jambo juu ya masuala ya uhalifu hasa wa mabenki unaotokea kwa njia ya Cyber Clime.
Watu
hao watatu ambao ni raia wa nchini Ugiriki kumbukumbu zao zinaonyesha
kwamba wamekuwa wakiingia na kutoka nchini Tanzania na kwenda nchi
mbalimbali za Afrika na Ulaya katika namna ambayo inaonyesha kuwa ni
wahalifu wa kimataifa kupitia mitandao.
Katika upekuzi watu hao wamekamatwa na vielelezo mbalimbali vinavyopashiria njama zao kama ifuatavyo:
- Muhuri mmoja wa kughushi ulioandikwa “Inspector General of Police DSM”
- Nyaraka mbalimbali za kughushi za Polisi Tanzania zinazowasaidia kwa lengo la kupata malipo ya bima nje ya nchi ambazo zina mihuri ya kughushi.
- Zimepatikana Kompyuta Mpakato (Laptops) zipatazo tisa ambazo watuhumiwa hawa huzitumia kwa ajili ya mawasilisano pamoja na uhalifu huo wa kimataifa.
- Zimekamatwa laini za simu za mkononi (Cheap) za kampuni ya simu ya Airtel ambazo baadhi zimetumika na nyingine hazijatumika.
- Aidha, zimekamatwa kadi mbalimbali za benki (Credit Cards) zipatazo 13 zinazotumika kutoa fedha, kuingiza fedha, au manunuzi mengine za ATM.
Pia
watuhumiwa hao wamekamatwa na vitabu vitano vyenye kumbukumbu za
majina, anwani, pamoja na namba za siri za wateja mbalimbali wa mabenki
mbalimbali kutoka nchi za Tanzania, Zambia, Afrika Kusini, Kenya,
Uingereza na Nigeria.
Uchunguzi
ziadi unaendelea kuhusu raia hao watatu kutoka nchi ya Ugiriki ili
kubaini mtandao wao na kugundua matukio mbalimbali ambayo wameyafanya.
Aina ya
uhalifu kupitia mifumo ya mitandao ambao wahalifu hao utumia akili
nyingi hasa kuunganisha namba za yaani digital ikiwemo umri wa mtu hasa
endapo wamegundua kutupia picha yako na majina yako
TAHADHARI KWA WANANCHI NA WAGENI WENGINE
Pamoja
na kuibuka na wimbi hili la wezi wa mtandao bado ni salama kuweka na
kutoa fedha katika mabenki hapa nchini. Hata hivyo kutokana na wimbi
hili la wizi kwa njia ya mtandao, ni muhimu sasa kuzuia uhalifu wa aina
hii kwa ushirikiano kati ya wamiliki wa mabenk na wateja wao.
Jeshi
la Polisi linashauri (pamoja na maelekezo mengine ya benki) njia sahihi
ya kwanza ya kuzuia ni kuhakikisha kwamba miamala yote inayofanyika
katika akaunti za benki ni lazima ifahamike kwa mteja kwa njia
zifuatazo:
- Mteja ajulishwe kwa simu ya mdomo ili kuthibitisha muamala.
2.Mteja
atumiwe ujumbe kwa kila muamala unaofanyika kupitia ujumbe mfupi wa
maandishi (SMS) kumjulisha mteja kiasi kilichotolewa, kiasi
kilichoingizwa au makato au maingizo yoyote kwa muda ule ule.
Aidha
tunawaomba wananchi waendelee kushirikiana na Jeshi la Polisi na
wasikubali kutoa nambari za akaunti zao kwa watu wasiohusika au nambari
zao za siri hata kwa mtu ambaye ni ndugu wa karibu sana.
Mara baada ya upelelezi kukamilika watuhumiwa hao watafikishwa mahakamani.
S. H. KOVA,
KAMISHNA WAPOLISI KANDA MAALUM,
DAR ES SALAAM.
Msamaji
wa Modeewji blog, endelea kuperuzi nasi tunajitahidi kukuletea makala
maalum itakayoelezea zaidi juu ya Cyber Crime hasa namna inavyotumika
kwenye wizi wa mabenki ambapo wahalifu hao wa mitandao wanavyofanya
uhalifu huo,
إرسال تعليق