Kambi ya wakimbizi wa Somalia ya Daadab
Umoja wa mataifa unasema kuwa haujapokea amri rasmi kutoka kwa serikali
ya Kenya ya kuutaka ufunge kambi ya wakimbizi ambayo ni makao kwa
maelfu ya raia wa Somalia.
Siku ya jumamosi makamu wa rais wa
Kenya William Ruto alisema kuwa amelipa shirika la kuhudumia wakimbizi
la umoja wa mataifa muda wa miezi mitatu ya kufunga kambi hiyo na
kuwasafirisha wakimbizi hao kwenda nchini Somalia.
Amesema kuwa la sivyo Kenya itachukua jukumu hilo mikononi mwake.
Baadhi
ya wanasiasa nchini Kenya wanaamini kuwa kambi hiyo imekuwa eneo la
kuwapa mafunzo wanamgambo wa Al shabaab ambao waliwaua karibu wanafunzi
150 wa chuo cha Garissa zaidi ya wiki moja iliyopita.
Post a Comment