Wasichana Wanaojiuza Nigeria Kutoa huduma ya Bure Siku Tatu Baada ya __?


Waswahili wanasema ahadi ni deni.. akina dada ambao wanafanya biashara ya kuuza miili yao Nigeria nao wanaahidi kutimiza ahadi yao ya kutoa huduma bure kwa wateja wao nchi nzima.
Chama cha wasichana hao ambao wanafanya biashara hiyo Nigeria waliahidi kwamba wako tayari kutoa huduma bure kwa mtu yoyote iwapo Rais Buhari atashinda Uchaguzi huo.. Kwa kuwa tayari Buhari kashinda wamesema watatoa huduma hiyo kwa siku tatu bure ili kumshawishi Rais huyo kuruhusu biashara hiyo kuwa halali kabisa kama ilivyo biashara nyingine.
Chama hicho ambacho kinaitwa NANP kimesema iwapo biashara hiyo ikihalalishwa itasaidia waweze kufanya biashara yao kwenye mazingira ya usalama zaidi hata wa afya zao.
Iliwahi kusikika pia kutoka Kenya ambapo wanawake wanaofanya biashara hiyo waliandamana mpaka kwa Mwanasheria Mkuu kutaka biashara yao ihalalishwe, watambulike na walipe kodi kama wafanyabiashara wengine tu.

Post a Comment

Previous Post Next Post