Waswahili wanasema ahadi ni deni.. akina
dada ambao wanafanya biashara ya kuuza miili yao Nigeria nao wanaahidi
kutimiza ahadi yao ya kutoa huduma bure kwa wateja wao nchi nzima.
Chama cha wasichana hao ambao wanafanya
biashara hiyo Nigeria waliahidi kwamba wako tayari kutoa huduma bure kwa
mtu yoyote iwapo Rais Buhari atashinda Uchaguzi huo.. Kwa kuwa tayari Buhari
kashinda wamesema watatoa huduma hiyo kwa siku tatu bure ili
kumshawishi Rais huyo kuruhusu biashara hiyo kuwa halali kabisa kama
ilivyo biashara nyingine.
Chama hicho ambacho kinaitwa NANP
kimesema iwapo biashara hiyo ikihalalishwa itasaidia waweze kufanya
biashara yao kwenye mazingira ya usalama zaidi hata wa afya zao.
Iliwahi kusikika pia kutoka Kenya ambapo
wanawake wanaofanya biashara hiyo waliandamana mpaka kwa Mwanasheria
Mkuu kutaka biashara yao ihalalishwe, watambulike na walipe kodi kama
wafanyabiashara wengine tu.
إرسال تعليق