Wakazi wa kata ya Nkololo bariadi mkoani Simiyu wanakabiliwa na
tatizo la ukosefu wa umeme kwa zaidi ya miezi miwili tangu ulipokatika
mwezi wa pili na kusababisha kupanda kwa ghalama za maisha na kuongezeka
kwa matukio ya wizi na uvunjaji wa nyumba unaotokana uwepo wa giza huku
wakishangaa shirika ya umeme (Tanesco) na wakala wa umeme vijijini
(REA) wakiendelea kutupiana mpira kana kwamba wote hawa husiki na suala
ilo bila kujali madhara wanayo yapata wananchi.
Wakizungumza na ITV iliyotembelea katika eneo ilo wakazi wa Nkololo
wamesema tangu umeme ulipo katika mwezi wa pili mwaka huu hadi sasa
hawajapatiwa ufumbuzi na wanapo piga simu Tanesco hakuna jibu wanalo
pata huku wananchi wakiendelea kuteseka kwa kukosa huduma hiyo muhimu.
Kwa upende wao baadhi ya viongozi wa halmashauri ya Bariadi
wamesema hali hiyo imesababisha kuongezeka kwa matukio ya wizi ujambazi
na uvunjaji wa maduka yanayo tokana na uwepo wa giza nene nyakati za
usiku na wamekuwa na wakati mgumu katika uongozi wao sasa wanatarajia
kupeleka kero katika baraza la madiwani.
Diwani wa kata ya Nkololo Masunguro Mbushi amesema ameshapeleka
kero hiyo kwa uongozi wa shirika la ugavi wa umeme Tanesco na kuahidiwa
kuwa litamalizika baada ya wiki mbili lakini hakuna dalili na ajabu
zaidi watu wanaendelea kukatwa fedha za huduma ya umeme bila huruma.
ITV ilifika katika ofisi ya shirika la Tanesco wilaya Bariadi
kumwona meneja Bwana Geogle Madaha ili kupata ufafanuzi wa kero hiyo
bila mafaniko baada ya ofisi kuwa zimefungwa kwa mapumziko marefu ya
sikuku ya pasaka na siku ya karume na tulipo mpigia kwa simu yake ya
mkononi alisema yupo mbali na ofisini lakini juhudui za kumtafuta
zinaendelea.(ITV)
إرسال تعليق