INASIKITISHA
 sana! Vijana wawili, Jumanne Omar (17) na Mgeni Rashidi Rajabu (16) 
(aliyekuwa mwanafunzi wa kidato cha nne Shule ya Sekondari Keko), Dar, 
wakazi wa Mtoni Madafu, Temeke wameuawa kwa kuchomwa moto na wananchi 
wenye hasira kali baada ya kudhaniwa kuwa ni wezi.
Marehemu Jumanne Omar enzi za uhai wake.
Tukio hilo la kinyama lilitokea wiki iliyopita Gongo la Mboto, Dar 
ambapo kijana aliyefahamika kwa jina la Hassan ambaye ndiye mkazi wa 
huko alidaiwa kuwafuata marehemu hao Mtoni Madafu na kuwaambia ametumwa 
na mama yake mzazi  aende akafanye vurugu kwa hawara ‘mchepuko’ wa baba 
yake.
Inadaiwa kuwa, Hassan akiwa na vijana wengine wawili, aliongozana na 
vijana hao kwenda Gongo la Mboto kwa mwanamke huyo ambaye ni mama 
lishe.Ndugu mmoja wa Jumanne anasimulia: “Walipofika kwa mama lishe huyo
 ambaye Hassan alidai ndiye mchepuko wa baba yake, waliagiza chakula. 
Walipomaliza kula yule mama aliwadai pesa, Hassan akasema hawana na 
hawatoi.
“Tunasikia yule mama akaamua kukusanya vyombo walivyolia chakula ili 
akaoshe, lakini ghafla Hassan alimpora simu na pesa za mauzo na kukimbia
 na wale wenzake wawili ambao ni wakazi wa hukohuko Gongo la Mboto na 
kuwaacha Jumanne na Mgeni.
“Ilibidi mama lishe apige kelele za mwizi, watu wakatokea na 
kumkamata Mgeni na kuanza kumpiga, baadaye wakamkata kisogoni kwa panga 
huku Jumanne akikimbia kuomba msaada na kujitetea kuwa wao si wezi naye 
akakamatwa na kuanza kupigwa.
Marehemu Mgeni Rashidi Rajabu enzi za uhai wake.
“Wakati wananchi hao wakiendelea kuwapiga vijana hao, alitokea dereva
 wa bodaboda ambaye alishauri kuwa vijana hao wachomwe moto mpaka 
wateketee.“Alikwenda kuchukua petroli   na kuja kuwamwagia kisha 
akawasha kiberiti na vijana wakaanza kuungua moto huku wakipiga kelele 
kuomba msaada.”
Ilidaiwa kuwa, baada ya kupata taarifa hizo ndugu walizunguka 
kutafuta miili ya vijana hao na kuikuta katika Kituo cha Polisi cha 
Stakishari, Ukonga, Dar na baadaye kupelekwa Hospitali ya Taifa 
Muhimbili kwa ajili ya uchunguzi kabla ya mazishi.
Dada wa Jumanne anasimulia: “Sisi tulipigiwa simu na mpangaji 
mwenzetu saa mbili usiku, yeye anafanya shughuli zake hukohuko Gongo la 
Mboto, akatuambia mdogo wetu anauawa kwa kuchomwa moto, tukashangaa sana
 na kujiuliza imekuwaje na nini kimempata.
“Tuliondoka hapa na kuanza kupita kwenye hospitali kubwa tukianzia 
Temeke, Mwananyamala mpaka Muhimbili hatukukuta mwili, tukaamua kwenda 
Polisi  Stakishari ndiyo tukakuta miili ya wawili. Inauma sana jamani 
mimi mpaka leo hii siamini.”
Naye baba mzazi wa Mgeni, Rashid Rajabu ambaye anaishi Zanzibar alisema:
“Kifo cha mwanangu kimeniumiza sana. Nakumbuka siku si nyingi nimetoka kumlipia ada ya mwaka mzima shuleni kwa sababu ilikuwa amalize kidato cha nne mwaka huu.
“Kifo cha mwanangu kimeniumiza sana. Nakumbuka siku si nyingi nimetoka kumlipia ada ya mwaka mzima shuleni kwa sababu ilikuwa amalize kidato cha nne mwaka huu.
“Naamini yote ni mipango ya Mungu japo mwanangu alikuwa kichwa 
darasani hata wanafunzi wenzake wameumia lakini hawanifikii mimi mzazi. 
Ngoja tuwaachie wahusika maana nimesikia suala hili limeshafika polisi,”
 alisema baba huyo.Miili ya vijana hao ambao iliharibika kwa moto, 
ilizikwa katika Makaburi ya Mtoni kwa Kombo, Jumatatu ya Aprili 13, 
mwaka huu.
Mwenyezi Mungu azilaze roho za marehemu mahali pema peponi. Amina.
Uwazi linaendelea kufuatilia sakata hili kwa kina ili kujua nini kilitokea kwa Hassan, yupo wapi na mama lishe alichukuliwa hatua gani.
Uwazi linaendelea kufuatilia sakata hili kwa kina ili kujua nini kilitokea kwa Hassan, yupo wapi na mama lishe alichukuliwa hatua gani.

إرسال تعليق