Mahakama
ya Nidhamu ya Umoja wa Mataifa imetoa hukumu ya kwamba adhabu ya
kusimamishwa kazi kwa Afisa wa ngazi ya juu wa Shirika la Umoja wa
Mataifa la Haki za Binadamu kwa kosa la kutoa taarifa iondolowe mara
moja.
Afisa huyo Anders Kompass, alitoa taarifa kwa mamlaka za
Ufaransa kwamba majeshi ya Ufaransa ya kulinda ya amani huko Jamuhuri ya
Afrika ya Kati walihusika kuwanajisi watoto.
Ataruhusiwa kurudi kazini mara baada ya shauri lake kupitiwa na maafisa wa ndani ya shirika hilo.
Umoja wa mataifa umekanusha kutaka kufunika tuhuma hizo.
Post a Comment