MAHAKAMA
Wilayani Bariadi Mkoa wa Simiyu, jana imemhukumu kulipa faini ya Sh.
2,000 tu au kwenda jela miezi sita, kada mmoja wa Chama Cha Mapinduzi
(CCM) wilayani humo, Ahamed Ismail, kwa kosa la matumizi mabaya ya
silaha yake.
Ismail alikumbana na hukumu hiyo jana Mei, 5, 2015 baada ya kusomewa mashtaka mawili. Shitaka la kwanza lilidai kuwa Aprili 22, mwaka huu, saa 10 jioni, alikwenda kwenye mkutano wa hadhara wa CCM katika Mtaa wa Isanga, huku akiwa na silaha aina ya bastola iliyokuwa ikionekana wazi.
Kosa la pili, ilidaiwa kwamba siku na tarehe hiyo hiyo, kiasi cha saa moja jioni, Ismail akiwa kwenye msafara wa Mbunge wa Jimbo la Bariadi Magharibi, Andrew Chenge, alitoa silaha ya moto hadharani kisha kufyatua risasi tatu karibu na Ofisi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Wilaya ya Bariadi.
Pamoja na maelezo mengine kadhaa, baada ya kusomewa tuhuma hizo, mshitakiwa alikiri makosa yote hayo mawili, na alipotakiwa na Mahakama kujitetea kabla hajatiwa hatiani kwa makosa hayo, akasema...
Habari zaidi soma=> Kada wa CCM aliyemimina Risasi mbele ya Ofisi ya CHADEMA Bariadi-Simiyu ahukumiwa kulipa Sh. 2,000/=

Post a Comment