Miezi
michache tu baada ya kumlaumu mamake mzazi kwa kumroga na kumfanya
apoteze fomu yake, Emmanuel Adebayor anayeichezea timu ya Tottenham
inayoshiriki ligi kuu ya soka nchini Uingereza, amejitokeza na kufichua
jinsi familia yake ilivyomfanya afilisike bila shukrani.
Kupitia ukurasa wake wa facebook, Adebayor ameeleza kuwa
"Nimekuwa
nikiziweka taarifa hizi kwa muda mrefu lakini leo nimehisi kuwa ni
muhimu kuwaeleza nanyi pia. Ni ukweli kuwa masuala ya familia
hayastahili kuwekwa hadharani lakini nafanya hivi ili familia nyingine
nzao zipate funzoi kupita yaliyonisibi. Aliandika
Anasema wakati
alipokuwa na umri wa miaka 17, aliutumia mshahara wake wa kwanza
kuijengea familia yake nyumba.Kama mnavyojua nilipokea tuzo ya mwanasoka
bora wa Afrika wa mwaka mwaka 2008.Nilimpandisha mama yangu jukwaani
kumshukuru yeye kwa mambo yote. Mwaka ule ule nilimleta London kwa ajili
uchunguzi wa afya yake.
Wakati binti yangu alipozaliwa
niliwasiliana na mama yangu kumweleza lakini alikata simu na sikujua ni
kwanini.Soma maoni yangu ya hivi karibuni watu wanasema mimi na familia
yangu twende tupate ushauri kwa mhubiri maarufu wa dini ya kikristo T.B
Joshua.Mwaka 2013 nilimpa mama yangu pesa ili aende kupata ushauri kwa
mhubiri huyo nchini Nigeria.
Alipaswa kukaa huko kwa wiki moja,
lakini siku mbili tu alipofika nilipokea simu kwamba ameondoka. Zaidi ya
hayo nilimpa mama yangu pesa nyingi kuanzisha biashara kupika pamoja na
bidhaa nyingine. Kiuhalisia niliwaruhusu kuweka jina langu na picha
yangu kwenye biashara hiyo hiyo ili waweze kuvutia wateja.
Ni kitu gani kingine mtoto wa kiume anaweza kufanya ndani ya uwezo wake kusaidia familia yake?
Miaka
kadhaa iliyopita, nilinunua nyumba huko East Lagon nchini Ghana kwa
dola milioni 1.2 za kimarekani. Nikaona ni sawa dada yangu mkubwa Yabo
Adebayor kuishi katika nyumba hiyo. Vile vile nilimruhusu kaka yangu
Daniel naye aishi kwenye nyumba hiyo.
Miezi michache baadae
nilifukuzwa kwenye nyumba niliyokuwa naishi ikianibidi kwenye hiyo
nyumba yangu. Kilichonishangaza niliona magari mengi kwenye barabara.
Kwa kweli dada yangu aliamua kuikodisha hiyo nyumba pasipo kunieleza.
Alimfukuza Daniel kwenye hiyo nyumba.
Mfahamu kwamba nyumba hiyo
ina vyumba 15. Nilipompigia dada yangu anipe ufafanuzi alichukua karibu
nusu saa kunishambulia na kunitukana kwenye simu. Nilimpigia mama yangu
anaelezee kisa kizima naye akafanya kama dada yangu alivyofanya. Hivyo
ni kama dada yangu alivyosema sina shukrani.
Kaka yangu Kola
Adebayor, anaishi nchini Ujerumani kwa miaka ishirini na mitano
sasa,safari zake zote za kurejea nyumbani mara nne ametumia gharama
zangu,kama hiyo haitoshi ninawasomesha watoto wake na kuwalipia gharama
zote kuhusiana na elimu yao.
Nilipokuwa nchini Monaco ,alinifuata
na kutaka pesa za kuanzishia biashra yake .Mungu pekee ndiye ajuaye
nilimpa kiasi gani cha kufungulia biashara yake,kama ukimuuliza biashara
hiyo iko wapi leo?
Masahibu hayakuishia hapo,kaka yetu Peter
alipoaga dunia nilimtumia Kola kiasi kikubwa cha pesa ili arejee
nyumbani,cha kushangaza hakutokea msibani ama siku ya maziko.na leo kaka
yule yule (Kola) anawaambia watu kuwa chanzo cha kifo cha kaka yetu
Peter ni mimi,linawezekanaje hili? Kaka huyu huyu alikwenda kwenye
gazeti la"The Sun" na kueleza habari za uongo kuhusiana na familia yetu
ili kujipatia fedha.
Wakatuma barua pia katika klabu ya mpira ya
Madrid nikafukuzwa.nilipokuwa nchini humo pia nilipata wazo kuwa ni
vyema kuwa na familia ya wana soka,hivyo nikahakikisha kaka yangu Rotimi
anajiunga na chuo cha mafunzo ya mpira huko Ufaransa. Miezi michache
tu,wachezaji ishirini na saba wa chuo hiyo aliwaibia simu za mkononi
wachezaji ishirini na mmoja .Sikuongea chochote kuhusiana na kaka Peter
Adebayor ,kwasababu hayuko nasi leo hii,Mungu ailaze mahala pema peponi
,amina.
Dada yangu sasa, Lucia Adebayor amekuwa na tabia ya
kuwaambia watu kuwa baba yetu amenitaka nimchukue dada huyu na kumpeleka
ulaya,lakini sababu kubwa hasa ni nini ya kumpeleka huko ulaya? Kila
aliyeko hapa yupo kwa sababu.
Nilirejea nyumbani Ghana nilipata
taarifa za kaka yangu anaumwa sana,niliendesha gari kwa kasi sana
kuelekea Togo ili kukutana naye na kumpa msaada anaostahili,nilipowasili
huko mama yangu akanikatalia kumwona na kunieleza kuwa ninachopaswa
kufanya ni kumpa mama yangu pesa nay eye ata maliza kila kitu.
Mungu
pekee ndiye ajuaye siku ile ile nikampatia mama yangu kiasi cha pesa
alichokitaka,lakini cha ajabu watu wanalalama kuwa sikufanya lolote
kuokoa maisha ya kaka yangu Peter.je mimi ni mpumbavu kiasi gani
niendeshe gari mpaka Togo bure bila ya sababu?
Nikaandaa mkutano
wa kifamilia mwaka 2005 ili tumalize tofauti zetu na matatizo
yanayotuzunguuka.nilipowauliza maoni yao wakanitaka kuwajengea nyumba
kila mmoja wao na mishahara mikubwa kila mwezi kwa kila mmoja wao.
Leo
hii niko hai wamejimilikisha kila kilicho change je nikifa
itakuwaje?kwa sababu zote hizi,itanichukua muda mrefu mno kuweka
mikakati na misingi yangu barani Africa.kila wakati ninajitahidi
kuwasaidia wahitaji,familia yangu wao huhoji kila nifanyacho na wote
huona nimefanya uamuzi mbaya.
Ikiwa leo ninaandika haya,sina lengo
la kuwaanika watu wa familia yangu.ninataka familia zingine za kiafrika
kujifunza kutokana na ninayoyapitia mimi. Asanteni sana.
Post a Comment