Ukiisikia
China na Sheria zake ni msumeno kweli, wakiandika hukumu yao kama ni
kunyongwa basi hakuna huruma itakayokuokoa.. wamefanikiwa kuzuia vingi
kutokana na Sheria zao kali walizopitisha kwenye nchi yao.
Dongguan ni mmoja ya miji ambayo inaongoza kuwa na viwanda vingi sana,
ishu ya Serikali ya China kuingiza kampeni mtaani ya kamata kamata kwa
kila mtu ambae anajihusisha na biashara ya kujiuza kumbe imeathiri
sehemu kubwa sana ya mapato ambayo huwa yanakusanywa kila mwaka kwenye
Jiji hilo.
Kwa
hesabu ya haraka wanasema hasara ya kuzuia biashara hiyo kwa karibia
mwaka mmoja ni Dola bil. 8 zimepotea, kuna Mahoteli makubwa ambayo
walikuta yanaruhusu wasichana kujiuza yalifungwa, sehemu nyingine ni
kama zilizokuwa zinatoa huduma za massage, kote kulifungwa kabisa !!
Haimaanishi biashara ndio imekwisha,
yani kuna wateja na watoa huduma hiyo ambao wanafahamiana kabisa,
Serikali imesimamia kila kitu mtaani lakini bado mambo yanaenda
chinichini, jamaa mmoja akasema yeye ni shuhuda.. aliunganishwa na
msichana anayejiuza, akalipia dola 160 baada ya kuhudumiwa kwa dakika
90.
Post a Comment