Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB – Bw. George Nyatega.
Na Mwandishi Wetu
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu
ya Juu (HESLB) jana (Ijumaa, Mei 1, 2015) imetoa mwongozo kwa wanafunzi
wahitaji wanaotarajia kuomba mikopo na ruzuku kwa ajili ya mwaka wa
masomo 2015/2016 unaotarajiwa kuanza miezi michache ijayo.
Kwa mujibu wa mwongozo huo, ambao unaanza kupatakikana leo katika tovuti ya Bodi (www.heslb.go.tz),
waombaji wote wamepewa takribani miezi miwili kuwasilisha maombi yao
kuanzia Jumatatu, Mei 4, 2015 hadi Jumanne, Juni 30, 2015.
Aidha, wanafunzi wote wahitaji wa
mkopo na ruzuku wanapaswa kufanya na kuwasilisha maombi yao kwa njia ya
mtandao kupitia mfumo maalum (Online Loans Application and Management
System) ulioanzishwa na HESLB kwa ajili ya kupokea maombi hayo. Mfumo
huo unapatikana kupitia tovuvi ya Bodi au kwa kufungua kiunganishi chake
(http://olas.heslb.go.tz).
Pamoja na mambo mengine, mwongozo
huo unafafanua kuwa waombaji wa mara ya kwanza (First Time Applicants)
wanapaswa kulipa ada ya maombi ya Tshs 30,000/- kwa na kisha kutumia
namba ya muamala (Transaction ID) kuingia katika mtandao na kuanza
kujaza fomu za maombi.
“Waombaji wa mara ya kwanza
wanapaswa kulipa ada ya maombi ya Tzs 30,000/- ambayo inalipwa mara moja
tu na haitarudishwa kwa nia ya M-Pesa,” inasema sehemu ya mwongozo huo
uloiotolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi hiyo.
Aidha, mwongozo huo umesisitiza kuwa
wanafunzi wenye mikopo na wanaoendelea na masomo katika taasisi
mbalimbali za elimu ya juu hawapaswi kuwasilisha maombi tena.
Bodi imewasihi waombaji na wadau wengine kuusoma na kuuzingatia muongozo huo wakati waote wanapofanya na kuwasilisha maombi.
HESLB ilianzishwa kwa sheria ya
Bunge na 9 ya mwaka 2004 na kuanza kazi rasmi mwezi Julai, 2005 ili,
pamoja na majukumu mengine kutoa mikopo kwa wanafunzi wahitaji
waliodahiliwa katika taasisi za elimu ya juu. Aidha, jukumu jingine la
Bodi ni kudai na kukusanya mikopo yote iliyotolewa kwa wahitimu wa
taasisi za elimu ya juu kuanzia mwaka 1994 wakati Serikali ilipoanza
kukopesha wanafunzi.
Post a Comment