Hiki ndicho kilichonifikia kuhusu nyumba ya Ali Kiba kuvamiwa usiku wa kuamkia leo.. (PICHA)

Reporter wa millardayo.com alikuwa mmoja ya watu wa kwanza kupewa taarifa juu ya tukio hili, akafika Kunduchi ambako Ali Kiba na mdogo wake Abdu Kiba wanaishi.
Nimeongea na Abdu Kiba, amesema yeye alikuwa Masaki, Ali akampigia simu kwamba kuna watu kama 15 hivi wamevamia nyumbani kwao.. waliovamia waliruka ukuta saa tisa usiku, wakavunja mlango wa sebuleni, wakakuta vijana wawili ambao wanaishi nao, wakawapiga na kuwalazimisha wawaoneshe chumba ambacho Ali yumo.. wale vijana wakajibu kwamba Ali hayupo, wakaulizia chumba chake wakaoneshwa chumba cha Abdu Kiba.
Wameingia chumbani wakamkosa Ali Kiba, wameiba vitu vingi vya sebuleni na chumbani pia, pamoja na pesa milioni 2 na nusu zilizokuwa chumbani kwa Abdu.
Askari walifika na kukagua, wakaondoka na kuahidi kwamba wanafanya upelelezi.
Wakati tukio lote linaendelea Ali alikuwa ndani kwenye chumba kingine, hawakuomuona.

Post a Comment

Previous Post Next Post