Maafisa nchini Iraq wanasema kuwa wanamgambo wa islamic state wamewaua
mamia ya watu wa yazidi waliokuwa wakiwazuilia eneo lililo kaskazini mwa
nchi.
Makamu wa rais nchini Iraq Osama al-Nujifi ameyalaani mauaji hayo akiyataja kuwa ya kikatili
Taarifa zilisema kuwa hadi watu 300 waliuawa kwenye wilaya moja iliyo magharibi mwa mji wa Mosul siku ya ijumaa.
Wanamgambo
wa islamic state walithibiti maeneo yaliyo kaskazini mwa Iraq kwa
karibu mwaka mmoja uliopita ambapo waliwaua na kuwashika mateka maelfu
ya watu wa Yazidi wakiwaita makafiri.
إرسال تعليق