Rais Jakaya Kikwete (pichani) ameahidi kuyashughulikia madai ya walimu kabla ya kuondoka madarakani.
Alitoa ahadi hiyo juzi jioni alipokuwa akizungumza na walimu zaidi ya 1,000 kutoka mikoa yote nchini.
Walimu walikutana katika Mkutano Mkuu wa Tano wa chama chao (CWT) unaoendelea.
Hata hivyo, Rais Kikwete aliwataka kuacha mara moja kushiriki
vitendo vya kuiibia serikali kwa kushirikiana kupiga ‘dili’ na wahasibu
wa wizara ya elimu na mafunzo ya ufundi.
“Madeni mliyoyataja kwenye risala yenu tutaendelea na kazi ya
kuyahakiki kwa kushirikiana na CWT na wakaguzi wa ndani,” alisema Rais
Kikwete.
Aliwatahadharisha kuwa endapo ukaguzi ukifanywa utawakuta pia walimu na kushitakiwa kwa makosa ya kuiibia serikali.
Alitumia fursa hiyo kuwaaga walimu wote nchini, huku akisisitiza
kuwa mambo, ambayo hakuyakamilisha, atayakabidhi kwa mrithi wake mara
moja.
Katibu Mkuu wa CWT, Alhaj Yahya Msulwa, alimuomba Rais Kikwete
kutekeleza mambo waliyomuomba kabla ya kuondoka madarakani mwishoni mwa
mwaka huu, ikiwamo kutatuliwa uhaba wa walimu na posho za kufundishia.
إرسال تعليق